Ofisa katika Kitengo cha Habari na Mawasiliano TGNP, Deogratius Temba, akikabidhi vifaa hivyo kwa wanakituo hicho. |
Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP), umepanua wigo
wa mawasiliano kwa makundi ya pembezoni hasa wanwake kwa kuwapatia vifaa vya
teknolojia ya habari na Mawasiano (TEHAMA) kwaajili ya kupashana habari katika
Kituo cha taarifa na maarifa Mkambarani Morogoro Vijijini.
Akikabidhi
vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 1.9, Ofisa katika
Kitengo cha Habari na Mawasiliano TGNP, Deogratius Temba, amesema kuwa shirika hilo limeamua kutoa vifaa hivyo
kwaajili ya kuhakikisha makundi yaliyoko pembezoni hasa wanawake wanafikiwa kwa
kupata taairfa sahihi kwa wakati muafaka na kuwawezesha pia wao kutoa taraifa
walizo nazo katika ngazi ya jamii.
“Huu ni
mradi unaowezesha sauti za jamii kusikika,
kuanzishwa kwa ‘Sauti ya Jamii’ kunawezesha sauti za wanawake wengi kupewa taarifa na
kutoa na kusikika, Tunajua hii itawezesha wanawake wengi kupaaza sauti zao na kupambana na matukio ya
ukatili wa kijinsia pamoja na changamoto nyingine zilizoibuliwa wakati wa
Utafiti raghibishi mwaka 2012 na tamasha la Jinsia la mwaka 2012 hapa
Mkambatani” alisema Temba
“Kwa mantiki hii TGNP imeona fursa kubwa ya kutumia ujumbe mfupi kama nyenzo ya kusaidia kuunganisha nguvu katika kuhabarishana na kuchukua hatua za kwajibisha mamlaka na kuleta mabadiliko chanya” aliongeza.
Sauti ya jamii itatumia teknolojia ya bulk SMS yaani kutuma ujumbe mfupi wa simu kwa kutumia computer kwa watu wengi zaidi ya 10,000 kwa wakati mmoja. Sauti ya jamii itasaidia kupashana habari kupitia kituo cha taarifa na maarifa cha jamii kwenda wa wadau mbali mbali wakiwemo wanaharakati waliohusika katika Utafiti wa mwaka jana, madiwani, Wanajamii wa Mkambarani, kamati mbalimbali za maendeleo Mkambarani, viongozi wa serikali za mtaa , kata hadi wilaya, madiwani na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
Makamu
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Mkambarani, Teresia Berege, alisema
kuwa kuwepo kwa Kituo hicho na vifaa hivyo vya kisasa kutasaidia kurahisisha mawasiliano, upashanaji wa taarifa
na kupata habari kwa haraka itakuwa ni ukombozi kwa watoto na wanawake na
kuwaweka katika mazingira bora ya kupata maendeleo.
Naye Diwani
wa kata ya Mkambarani, danile Shawa alisema kuwa wanaharakati wa Mkambarani
wanapaswa kutumia vizuri vifaa vilivyotolewa na TGNP ili vilete ufanisi na
maendeleo kwa wakazi wa kata hiyo.
“ninawashauri
mtumie vema hivi vitu, kwa hapa kwetu Mkambarani hii ni fursa ya pekee,
tumepiga hatua sasa, tekonoljia ilikuwa nyuma sasa TGNP imewawezesha mnakwenda
na wakati, mtumie vizuri kwa uaminifu na unagalifu na msitume taarifa ambazo
hazina ukweli” alisema Diwani.
Chanzo:the habari
Chanzo:the habari