Wednesday, June 12, 2013

MAREKANI YADAIWA KUPEKUA MITANDAO DUNIANI

 

Shirika la Habari la Reuters limeripoti kuwa Wizara ya Sheria nchini Marekani imeanzisha uchunguzi kwa kile kinachosemekana ni ufichuaji wa taarifa za siri uliofanywa na mtaalamu wa zamani wa mitambo ya komputa katika shirika la ujasusi la Marekani,Edward Snowden.

Snowden alijitambulisha baada ya kufichua kuwa mashirika ya ujasusi nchini Marekani hufanya udukuzi kote dunini kwa kutumia mbinu ya kiteknolojia ya siri kuchunguza mawasiliano ya simu ya watu,barua pepe na mawasiliano mengine.

Ufichuzi wa Edward Snowden kuhusu shughuli hizo za kisiri zinazojumuisha kudukua mitandao na mawasiliano ya simu,umezusha wasiwasi kote ulimwenguni kuhusu kiwango cha ukusanyaji wa taarifa hizo za kijasusi Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza,William Hague,anatarajiwa kutoa tamko rasmi bungeni leo kuhusu tuhuma kwamba mashirika ya kijasusi ya Uingereza yalitumia data iliyokusanywa na mashirika ya kijasusi ya nchini hapo kubadili sheria kali kuhusu taarifa za siri.

Kwenye mahojiano na jarida la Guardian,Edward Snowden alisema kuwa wamarekani wanahujumu mamlaka ya serikali na kutishia demokrasia,hatua ya mtalaamu huyo wa teknohama imesababisha wasiwasi kuhusu uwezo wa Marekani kukusanya taarifa za kijasusi ambao anasema ni mkubwa.

Aliendelea kuliambia jarida hilo kuwa jambo inalofanya Marekani ni la kutisha,akiongeza kuwa wao huvamia mitambo na pindi mtu anapowasha mtambo wake wanaweza hata kuutambua mtambo wenyewe na mtu anayeutumia.

Popular Posts

Labels