Rekodi hii imevunja ile ya mwaka 2012 ambayo ilikuwa na ujumbe mfupi bilioni 19.
Kwa mujibu wa Whatsapp, ni kwamba ujumbe mfupi wa maneno bilioni 10 uliopokelewa na watumiaji bilioni 17, kumekuwa na uwiano wa ujumbe mmoja kutumwa kwa watu kumi kwa kutumia program hiyo.
Whatsapp inayotumika katika simu za mkononi za iOS, Android, Windows , BlackBerry, Asha, Symbian n.k kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno,picha,audio na video imefanikiwa kuvunja rekodi yake,na kuweka ushindani na mitandao jamii ya Facebook na twitter katika kipindi cha miezi sita,ambapo kwa sasa Whatsapp inawatumiaji wapatao milioni 200.
Hatua hii imeonekana kuizidi huduma ya BBM inayotumiwa na simu za BlackBerry ambayo ndiyo iliyokuwa ikiongoza,ambapo kampuni hii toka Canada inawatumiaji milioni 60 wanaotuma na kupokea ujumbe bilioni 10 kila siku.
Hata hivyo Whatsapp bado inaushindani kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Uchina ambako kuna program tumishi ijulikanayo kwa jina la Wechat ambayo inawatumiaji milioni 300 kati ya hao milioni 40 wanaishi nje ya China.