Jumuia ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini Tanzania kupitia
mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter imezindua rasmi shindano la
kusaka kampuni zinazotoa huduma na bidhaa mbovu kwa wateja nchini
Tanzania. Jumuiya hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo
wanasheria, wanaharakati, waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa,
wafanyabiashara na wateja wa huduma na bidhaa mbalimbali nchini
Tanzania.
Lengo la jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara nchini kutoa
huduma na bidhaa bora kwa wateja na kuwakumbusha umuhimu wa wateja.
Kauli mbiu ya wanajumuiya hao ni Mteja ni Mfalme. Katika wiki ya kwanza
tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa katika
shindano hilo kwa wateja wao kuwasilisha malalamiko yao. Kwa taarifa
zaidi kuhusu ni fuatilia akaunti ya Twitter @hudumambayatz au kundi la
Facebook linalojulikana kama HUDUMA BONGO.
Ili kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai (yenye
mawasiliano mara kwa mara) katika mtandao wa Twitter au Facebook na
kujiunga na jumuiya hiyo. Mara tu utakapowasilisha kero yako utaifanya
kampuni unayoilalamikia kuingia katika mchuano mkali wa kumsaka bingwa
wa huduma mbovu kwa wateja nchini.
Huduma Bongo inatoa wito kwa makampuni yote kuboresha huduma na
bidhaa zao ili kuweza kuwapatia wateja kilicho bora zaidi katika soko
hili la ushindani. Imetolewa na Mshauri wa Habari wa Huduma Bongo hudumabongo@gmail.com
Chanzo:thehabari