Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania jana ilianza kuendesha mkutano wa kimataifa kuhusu usimamizi na utekelezaji wa huduma ya simu za mkononi kwa kutumia kadi moja ya simu kwa mitandao yote bila kuwa na simu kadi nyingi za mitandao tofauti.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,Profesa John Nkoma, alisema kadi moja ya simu ya mkononi inaweza kutumika katika zaidi ya mtandao mmoja wa simu kama mteja atataka kuhama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila kununua kadi nyingine ya simu kama ilivyozoeleka.
Alisema lengo la mkutano huo ni kutaka kujadili kwa kina utekelezaji na usimamizi wa huduma maalum ya mawasiliano ya simu ambapo mtumiaji wa simu ya mkononi anaweza kutumia kadi moja tu kama atataka kujiunga na mtandao mwingine.
Huduma hiyo inatarajiwa kuanza mapema mwakani baada ya maandalizi na michakato yote,Huduma hii imeshaanza kutumika nchini Kenya tangu Aprili mwaka jana
Friday, November 16, 2012
Popular Posts
-
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeingilia kati wizi wa fedha kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeibua hofu kubwa katika s...
-
Itakumbukwa Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu katika hotuba yangu niliyo iwasilisha kwa wanausalama mitandao tulipo kutana jijini Johan...
-
Upungufu wa usalama wa herufi za siri za takriban simu milioni 900 umewapa wadukuzi fursa ya kudhibiti simu za android kote duniani...
-
Wabunge wa Tanzania wameibana serikali wakiitaka iboreshe muswada wa sheria ya mifumo ya malipo ili kuzibana kampuni za simu na mabenki,kuto...