Wednesday, November 14, 2012

WATEJA WA SIMU TANZANIA KUHAMA MTANDAO BILA KUBADILIA NAMBA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaandaa utaratibu wa kuanzisha mfumo mpya wa kuhama mtandao bila ya kubadili namba ya simu(MNP) na kuhamia mtandao mwingine.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,Prof.John Nkoma anasema mfumo huo utawasaidia watu wote wanaotumia simu nchini humo waliokuwa wanashindwa kuhamia mtandao mwingine kwa hofu ya kubadili namba ya simu,lakini baada ya kuzindua mfumo huu watu watahama mitandao kwa urahisi bila kubadili namba za simu.

Anafafanua kuwa mfumo huo utasaidia kuleta ushindani kwa makampuni ya simu na kuleta faida kwa wateja,pia makampuni hayo yataweza kuongeza ubora wahuduma kwa wateja wao.

TCRA imeandaa makutano wa kimataifa ambao utahudhuriwa na watu zaidi ya 100 wa kuzungumzia suala hilo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania,Prof.Makame Mbarawa.

Mkutano huo wa siku mbili unaotarajiwa kuanza kesho umeandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mawasiliano Duniani (ITU) na utahudhuriwa na wawakilishi mbalimbali kutoka duniani kote zikiwemo nchi za Afrika Mashariki

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo aliwataka wananchi kununua vinga'amuzi mapema ili kuondokana na usumbufu ambao unaweza kujitokeza baada ya kuhamia katika mfumo wa digital Disemba 31 mwaka huu.

Popular Posts

Labels