Wadau kutoka kampuni na mashirika mbalimbali nchini Tanzania wameshauri kutolewa elimu zaidi kuhusu matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama) na ufanisi wake ili kuleta tija kwa watanzania wengi.
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa warsha ya Teknohama iliyotolewa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,wadau hao walisema ni muhimu kwa wadau wengine ikiwamo serikali kuandaa mafunzo kama hayo kwani kuna mambo mengi ya msingi ambayo bado yanasumbua katika matumizi sahihi na ufanisi wa Teknohama.
Mmoja wa maofisa wa ubalozi wa Marekani Jeffrey Shrader alisema waliandaa warsha hiyo kwa sababu ya kukua kwa kiasi kikubwa kwa Teknolojia ulimwenguni hivyo ni vyema kuwaelimisha wengine ambao hawafahamu.
Katika warsha hiyo wakufunzi mbalimbali walitoa mada zinazohusiana na Teknohama ikiwemo ulinzi wa mawasiliano kama vile komputa na simu,mfumo wa uendeshaji wa mambo ya kuchukua na kutumia taarifa katika mitandao.
Popular Posts
-
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeingilia kati wizi wa fedha kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeibua hofu kubwa katika s...
-
Itakumbukwa Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu katika hotuba yangu niliyo iwasilisha kwa wanausalama mitandao tulipo kutana jijini Johan...
-
Upungufu wa usalama wa herufi za siri za takriban simu milioni 900 umewapa wadukuzi fursa ya kudhibiti simu za android kote duniani...
-
Wabunge wa Tanzania wameibana serikali wakiitaka iboreshe muswada wa sheria ya mifumo ya malipo ili kuzibana kampuni za simu na mabenki,kuto...