Facebook
wametangaza kitu kipya kwa simu za Android walichokipa jina la Home.
Kwa muda mrefu kulikuwa na uvumi kuwa Facebook wanajiandaa kuja na simu
yao mpya na hata siku za karibuni ilipotangazwa kutakuwa na tamko toka
Facebook uvumi ulisambaa kuwa wanatangaza simu yao mpya lakini haikuwa
hivyo.
Mark
Zuckerberg, CEO wa Facebook amesema lengo hasa ni kufanya unapowasha
simu yako kitu cha kwanza kinachotokea ni watu ulionao Facebook ambapo
utatokea ujumbe wa kukufahamisha ujumbe waliokuandikia, maoni na hata tags
na utaweza kujibu bila kufungua application yoyote. Yote hii ni kwa
ajili ya kuingia katika mfumo wa matangazo kupitia mobile web kwani ni
sehemu pekee ambayo Facebook haijaweza kuweka ads zake.
Android ambayo
kwa siku za karibuni imekuwa na watumiaji wengi duniani inaonekana kuwa
sehemu pekee ambayo Facebook inaweza kuanzisha utaratibu wa matangazo
kwa gharama nafuu kulinganisha na kama wangeamua kuja na simu zao
wenyewe.
Nini Utaweza Kufanya
Pamoja na kuwa na uwezo wa kusoma kila kinachoendelea kwenye account yako ya Facebook pale unapowasha simu, utaweza pia kutuma message wakati ukiendelea kutumia program tumishi nyingine kama Whatsapp au Keek kwa kutumia kitu kilichopewa jina la “Chat Heads”. Ikitokea ukapata message kwa mfano wakati unatumia Instagram, picha ya aliekuandikia itatokeza kwa juu na utaweza kujibu kwa kubofya bila kuacha ulichokuwa unakifanya.
Utaipataje?
App hii imeanza kupatika katika Google Play Store kuanzia April 12. Kama tayari unayo Facebook Messenger au Facebook tumishi yoyote utaombwa uijaribu Home. Ukishaiweka na kuanza kuitumia utagundua kitu kinachoitwa “Chat Heads” ambayo inachukua nafasi ya Facebook Messenger.
Simu Gani Zitakuwa Nayo:
Simu zitakazoanza nayo ni HTC One, HTC One X, HTC One X+, Samsung Galaxy S3, Samsung Galaxy S4, na Samsung Galaxy Note II. Simu nyingine zitaongezwa baadae.
Ili kuondokana na usumbufu wa kuiweka kwa kuipakua kwenye Google Store, simu zitakazoanza kutengenezwa baadae zitakuwa zinayo Home moja kwa moja na kwa kuanza HTC watakuwa wa mwanzo kuiweka Home katika simu zao zinazotoka hivi karibuni.
Chanzo:Tanganyikanblog