Friday, April 26, 2013
UNAVYOWEZA KUJILINDA NA PACHIKO AMA PICHA USIZOZIHITAJI KWENYE FACEBOOK ANGALIA HAPA
Kumekuwa na changamoto ya kujilinda na watu ambao wanaweza kukuwekea maelezo ama kukutagg picha usiyoihitaji kwenye timeline yako kwenye facebook iwe ni picha ama ni taarifa mbaya ama usizozihitaji.Na utagundua ya kwamba kuna watu ambao hata huwezi amini kama kweli wao wameweka picha zilizo kinyume na maadili na hii imekuwa ikiwakera wao ama watu wanaowasiliana nao kwenye mtandao wa facebook.
Kama inavyoonekana katika picha hapo juu ukifuata hatua hizo itakusaidia kujilinda kwanza ingia kwa timeline yako kulia mwa ukurasa ama timeline yako kuna kialama kinaonekana kama nyota ukishusha chini kasa yako ya mouse unaenda mahali pameandikwa privacy setting bofya hapo na utatokea ukurasa ambao kushoto kuna maelezo bofya palipo andika Timeline and Tagging.
Baada ya hapo utatokea ukurasa mwingine kulia kwake kuna maandishi meusi yameandikwa who can add things to my timeline hapo kuna mahali pa kuchagua Friends ama Only Me,kama ni friends ina maana rafiki yako yeyote anaweza kukuwekea jambo kwenye timeline yako maana hujaizuia,kama ni only me ina maana wewe tu ndo unayeweza kuweka jambo kwa hiyo utaamua angalia kielelezo namba tatu.
Pia kuna mahali pameandikwa Review Posts friends before they appear on your timeline hapo kuna Enable na Disable hapo utachagua enable maana yake uone kwanza wewe ndo itokea kwenye timeline yako vinginevyo utachagua disable kila rafiki yako aweza weka jambo kwenye timeline yako bila wewe kujua kama wewe huja login.
Hatua nyingine ni suala la kujilinda na picha usizozihitaji zitokee kwenye timeline yako kama mtu amekutagg hatua ni zile zile za mwanzo baada ya kuingia kwenye ukurasa wa privacy setting kuna mahali pameandika timeline and tagging angalia kielelezo namba nne hapo kuna Enable na Disable hiyo nayo inafanyakazi sawa sawa na pachiko hata kama hujalogin,fuatilia vilelezo vya picha kama zinavyoonekana juu.
Kumbuka baada ya kuweka setting hizi facebook watakuwa wanakutumia ujumbe kwa anuani yako ya barua pepe na kwenye timeline yako ukiwa na picha ama maelezo(jambo)ambalo limetumwa kuonekana kwenye timeline yako wewe utaliona kwanza ndo utaamua hiyo picha ama jambo lionekane kwanye timeline yako,pia unaweza hata kujiondoa kwenye hiyo tagg.
Popular Posts
-
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeingilia kati wizi wa fedha kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeibua hofu kubwa katika s...
-
Itakumbukwa Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu katika hotuba yangu niliyo iwasilisha kwa wanausalama mitandao tulipo kutana jijini Johan...
-
Upungufu wa usalama wa herufi za siri za takriban simu milioni 900 umewapa wadukuzi fursa ya kudhibiti simu za android kote duniani...
-
Wabunge wa Tanzania wameibana serikali wakiitaka iboreshe muswada wa sheria ya mifumo ya malipo ili kuzibana kampuni za simu na mabenki,kuto...