Monday, March 5, 2012

TAHADHARI YA UTAPELI:WIZI WA FEDHA KUPITIA "MOBILE BANKING"

Tahadhari ya utapeli: Wizi wa fedha kupitia "mobile banking"
“Ujumbe ufuatao nimeupokea kwenye e-mail kutoka kwa mtu ninayefahamiananaye.

Leo yamenifika, na ninapenda kutoa tahadhari hii kama hili halijawahikukumba. Leo asubuhi kuna jamaa alinipigia simu akidai kuwa anatoka kitengo cha NMB mobile banking akaniambia kuwa airtel wanatoa bonus kwa wateja wazuri wanaotumia service hiyo. Sasa bila kujua hili wala lile nikatoa taarifa za simu yangu na hata za account yangu.

Guess What?
Baada ya muda nikarealise kuwa line yangu imekuwa blocked na ndipo niliposhtuka na kujua kuwa nimeliwa!
Nilipiga simu kwa Bank Manager na kumweleza suala hilo na baadaye
alinidhhirishia kuwa account yangu imekombwa yote. Hivyo nikamwambia wai-block, kitu ambacho pia kilikuwa kinawapa shida kwa sababu line ilikuwa imeshachakachuliwa. 

Kama isitoshe, wakaanza kupiga simu kwa watu ambao awali walitaka niwape namba tano za watu ninaowapigia simu mara kwa mara,wakiwataka hao watu wanitumie pesa na kwa sababu simu ilionyesha kuwa inatoka kwangu wengine walikuwa karibu waanze ku-act. Kwa hiyo ni kuwa zile information za simu yangu ziliwasaidia ku-disable line yangu toka kwenye simu card yangu na na kuziweka kwenye simu card yao maana pia walihitaji ICC number ya sim card yangu, hivyo kuweza kuwasiliana na watu waki-impose kuwa ni mimi. Pili details za benki ziliwapa access kwenye account yangu na kuikwangua yote.

Kwa hiyo ndugu, kama hujawahi tokewa na hili au ulikuwa unalisikia tu kwa mbali leo hii mimi ninakuwa shahidi kwako na tafadhali usotoe taarifa zako zozote kupitia simu kama nilivyofanya mimi. Teknologia ina faida na hasara zake kwa hiyo siyo mbayo kushiriki vyote ila pale iwezekanapo jaribu
kuepuka hasara. Kama utataka kujua mbinu waliyotumia unaweza kuuliza nikujuze ili uwe makini kitokea mtu akakupigia simu kama hiyo.
Mungu awabariki sana !
Wenu Mhanga wa Teknolojia”

Popular Posts

Labels