Kutoka Kushoto Gerald Masatu,Mtangazaji Maduhu,Brown Nyanza(IFM),Mama Kagize,Johnson Kuga Mzirai na Jonathan Mnyela |
Monday, August 6, 2012
WADAU WA KIPINDI CHA MAISHA NA TEKNOHAMA MORNING STAR RADIO
MASWALI NA MAJIBU KUHUSU UHARIFU KWA MITANDAO
Kumekuwa na ongezeko kubwa la uhalifu kwa njia ya mtandao kutokana na kukuwa kwa tekinolojia mbalimbali za mitandao na kuongezeka kwa maarifa kwa baadhi ya watu wanaofanya shughuli mbalimbali kwa njia ya mtandao , katika watu hawa kuna wema+ na wale ambao si wema wanaotumia ujuzi wao huu kwa ajili ya kufanya uhalifu mbalimbali .
MTANDAO NI NINI?
Ni muunganisho wa vifaa mbalimbali vya mawasiliano unaosababisha vifaa hivyo kuwasiliana au watu wanaotumia vifaa hivyo kuwasiliana kwa nia ya kupata taarifa , kuhifadhi , kuchapisha au kufanya shuguli nyingine yoyote kwa njia ya mtandao .
Mtandao ni sharti kuwe na muungano fulani, kama simu ya mkononi , kompyuta ,luninga za digitali na vifaa vingine mbalimbali.
UHALIFU KWA NJIA YA MTANDAO NI NINI?
Ni pale mtu au kundi la watu wanapotumia njia mbalimbali za kimtandao kutenda makosa , hii inaweza kuwa wizi kwa njia ya mtandao inaweza kuwa hela , wizi wa taarifa na masuala yanayohusiana na suala zima la wizi , kudanganya watu watembelee tovuti Fulani kwa ajili ya kuwaibia taarifa zao , kuchapisha taarifa za uwongo ,kudownload (kupakua) program au muziki bila kununua au kwa kutumia program zilizokatazwa ,kutokufuata sheria na taratibu za nchi au eneo husika pale tunapotumia mtandao unapokuwa hapo .
UHALIFU WA MTANDAO UNA MIPAKA?
Uhalifu wa mtandao una mipaka kutegemeana na sheria au taratibu za sehemu ambayo mtu anatumia kwa wakati huo , kwa mfano kuna baadhi za nchi sheria zake za mtandao haziruhusu kutembelea au kutafuta vitu Fulani kwa njia ya mtandao ukifanya hivyo unakuwa umefanya kosa ,lakini uhalifu unaweza kufanyika mtu akiwa popote na saa yoyote endapo ameunganishwa kwenye mtandao .
SHERIA ZINASEMAJE KUHUSU UHALIFU WA MTANDAO?
Kama nilivyosema inategemea na mtu alipo na jinsi uhalifu ulivyofanyika , kuna baadhi ya nchi hazina sheria za masuala ya mitandao haswa inayohusu mawasiliano ya kimataifa(Internet), mtu anapokuwa kwenye nchi hiyo akafanya uhalifu sehemu nyingine ni ngumu kumtia hatiani au sheria za nchi husika zinapokuwa sio nzuri zinavutia zaidi wahalifu kujihifadhi au kutumia mitandao ya nchi hiyo kufanya uhalifu dhidi ya maeneo mengine ya dunia .
TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI TUKO WAPI ?
Mpaka sasa hakuna sheria moja ya masuala ya mawasiliano kwa jumuiya ya afrika mashariki kila nchi ina sheria zake ndogo ndogo Kwa Tanzania kuna EPOCA ambayo inagusia zaidi mawasiliano ya elekitroniki ,na kuna kikundi cha kupambana na uhalifu kwa njia ya mtandao kinachoitwa CERT .
SASA TUFANYAJE?
Nchi inapokuwa na sheria zake za mawasiliano haswa ya mtandao inapendeza na wengine haswa kampuni zinaweza kuandaa sera zao za mawasiliano kutumia muongozo wa nchi husika , sasa hivi kwa kampuni na mashirika hapa Tanzania yamekuwa yanapata tabu kuandaa sera zao za mitandao kutokana na kukosekana kwa sheria hizi za nchi .
Hata kama nchi haina , wewe kama kiongozi wa sherika au kampuni unaweza kuandaa muongozo wa mawasiliano ndani ya idara yako au kampuni yako itakayoongoza wafanyakazi na wageni wengine wanaotumia vifaa vya kazini kwako kwa ajili ya mawasiliano ili waweze kufuata taratibu na wanaweza kujiepusha na uhalifu mbalimbali kwa njia ya mtandao .
Miongozo hii inahusiana na matumizi ya vifaa pale anapoanza kutumia mtandao au anapoleta vifaa vyake kuunganisha , au anapotoa maoni katika mitandao ya kijamii , kuangalia picha , kushusha vitu mbalimbali , haki miliki na mengine mengi.
Na: Bupe Berrums bberrums@gmail.com-Wanabidii
Popular Posts
-
Picha na Salim Kikeke Kuanzia sasa kudanganya kwamba mtu hakupata ujumbe wako wa WhatsApp itakuwa historia, au kud...
-
1.Kutune Gitaa /Kutafuta Ufunguo wa Sauti ya Gitaa Kulikuwa na wakati ambapo bei ya vifaa vya umeme kwa ajili ya kutafuta ...
-
Mtaalamu wa masuala ya usalama kwenye Mtandao Yusuph Kileo akiwasilisha mada Itakumbukwa katika mkutano uliofanyika mapema mwezi h...
-
Apple wametoa Sasisho la Program Endeshi ya iOS 12.2 kwa ajili ya iPhone, iPad, and iPod toleo ambalo litawezesha wenye vifaa vya hivy...
-
Facebook is developing a new smartphone app to track the location of users in an effort to target them with localised adverts, acc...
-
Tokea LAPTOP zimeanza kuingia sokoni zimekua sehemu ya maisha yetu ya kila siku . Mwanzoni hazikua zinapendeza sana , Kubwa na Gha...
-
Idara ya uwakili ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani imesema kuwa Utoaji wa semina na makongamano kupitia mtandao wa intaneti u...
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akibofya kompyuta kuzindua huduma ya WiFi ya bure kwenye Kituo cha Mabasi cha Sinza, wi...
-
Wakati ugonjwa wa Ebola ukiendelea kuwa tishio katika baadhi ya nchi za Afrika magharibi, Wataalam wa afya nao wameendelea kuweka jitih...
-
Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Tekinolojia nchini Tanzania imeahidi kutoa msaada kwa shirika la posta nchini humo ili liweze kuwa shi...