Friday, October 26, 2012

TCRA YASEMA INAZINGATIA VIWANGO VYA SIMU TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Profesa John Nkoma,amesema Tanzania inazingatia viwango vya simu vinavyoingizwa Tanzania tofauti na jamii inavyofikiria.

Mkurugenzi huyo amesema hayo alipokuwa akikabidhi leseni mbili za kutoa huduma ya mawasiliano kwa kampuni ya Telesi hivi karibuni jinini Dar es salaam ambapo alieleza kuwa simu zote zinazoingizwa nchini zinafanyiwa uchunguzi ili kuhakikisha zina viwango vinavyotakiwa.

Nkoma amesema Tanzania haiwezi kuwa dampo la soko kwa simu zisizo na ubora kwa kuwa harakati zinazofanywa na nchi za Kenya na Uganda za kuzuia simu zisizo na ubora zilianza kutekelezwa nchini nchini.

Alisema iwapo wataamua kuhakikisha simu zinazoingizwa ziwe ni zile zenye ubora wa juu zaidi,hatua hiyo itawafanya baadhi ya watanzania kushindwa kumiliki simu kutokana na simu hizo kuuzwa kwa bei kuanzia shilingi 500,000 za kitanzania.

Popular Posts

Labels