Saturday, October 10, 2015

IFAHAMU NJIA MADHUBUTI YA KUKABILIANA NA UHALIFU MTANDAO


Tukio la kipekee katika anga ya usalama mitandao ambalo limekualiki azimishwa kila mwaka katika mwezi wa Oktoba ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa maswala ya usalama mitandao duniani kote. Na imani Mwaka huu Tanzania itauchukulia mwezi huu kinamna ya kipekee ili kuweza kukuza uelewa kwa watu wake Tukio ambalo nategemea makampuni mbali mbali na maeneo mengine yataandaa program mbali mbali za kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao ili kuweza kufikiwa malengo yaliyokusudiwa na wanausalama wote mitandao duniani kote.
Aidha, inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo la uhalifu mtandao.

 Tatizo kubwa kubwa ni kuwa njia hizi zimekua zikiishia katika maandishi baada ya kujadiliwa na wanausalama mitandao ambapo mimi binafsi nilikua miongoni mwao.

 Kwa kupata elimu hii wale wote waliokua wakifanya uhalifu mtandao pasi na kujua wanakua na ufahamu wa kutosha na hatimae kundi hili linakua limeondokana na uhalifu mtandao. Aidha, kundi la pili ambalo ni lile linalofanya uhalifuu huu wa mtandao wakiwa hawana namna kwa kutokujua athari zake baada ya kujua athari za uhalifu mtandao kwao na kwa wengine na pia kujua njia mbadala wanazoweza kutumia kuepukana na uhalifu huu kupitia elimu ya uelewa ya usalama mitandao kundi hili linaweza pia likapunguzwa hadi asilimia 84% kwa mujibu wa wataalam wa usalama mitandao.



Kundi la mwisho ambalo ni wahalifu wanaofanya uhalifu huu makusudi ingawa wanajua wakifanyacho na hawana utayari wa kuepukana na uhalifu huu mtandao nalo linapunguzwa nguvu kwani watumiaji mitandao wanakua na uelewa wa namna wahalifu hawa wanavyo fanya uhalifu na njia sahihi za kujilinda hatimae kundi hilipia linakosa watu wengi wanaoweza kuingia katika mtego wao wa uhalifu mtandao na kupungukiwa kasi na nguvu ya usambazaji wa uhalifu huu.



Inaaminika asilimia zaidi ya 37% ya wahalifu wa kundi hili la tatu wanapokosa watu wanoweza kuingia mtegoni wanajikuta wanakata tama na kujishughulisha na mambo mengine tofauti na uhalifu mtandao.



Kumekua na wimbi kubwa la makampuni mengi mbali na kua na teknolojia nzuri ya kuzuia uhalifu mtandao bado yameendelea kugubikwa na uhalifu mtandao kutokana na kutowekea mkazo swala hili la kukuza uelewa wa maswala haya ya usalama mitandao. Pia mataifa mengi yameendelea kujipanga kwa kua na vitengo kadhaa vya udhibiti uhalifu pamoja na kua na sharia sahisi za kudhibiti uhalifu huku bado wimbi kubwa la wahalifu mtandao bado likiendelea kua kubwa.

Tatizo ni kukosekana na njia sahihi na namna madhubuti ya kuendea njia hii ya kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao ambapo kama nilivyo fafanua awali ingeweza kabisa kupunguza kwa kiasi kukubwa swala hili la uhalifu mtandao.



Kumekua na jitihada nyingi za kuhamasisha kuanzia ngazi ya mtu binafsi, Makapuni , Nchi, Bara na hatimae Dunia nzima kujenga tamaduni ya kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao ili kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu unaoendelea kukua kwa kasi hivi sasa.



Swali linaloulizwa ni kwamba pamoja na jitihada nyingi  za wanausalama mtandao ambapo hadi sasa pamoja na mambo mengine, tayari kuna mwezi wa Kumi ambao unafahamika kama mwezi maalum wa maswala ya uelewa wa usalama mitandao yaani “OCTOBER" – Cybersecurity Awareness Month”  na kupatikana kwa tamthilia maalum ambazo zipo kukuza uelewa wa usalama mitandao.



Jibu ni kwamba, Jitihada hizi zimebaki kwa wanausalama mitandao na wananchi wakawaida bado imekua ni vigumu sana kufikiwa na kuelewa pamoja na kua miongoni mwa jitihada hizi.



Wengi bado wamebaki wakijua swala la ufahamu na uelewa wa maswala ya usalama mitandao ni swala la wanausalama mitandao pekee huku wengine wakiamini pia wana TEKINOHAMA ndio pia wanausika.



Inasahaulika kabisa swala la kubaki salama kimtandao ni swala linalo takiwa kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi sawa kabisa na swala la ulinzi wa uhalifu mwingine wowote. Tumekua na utamaduni wa pamoja na mambo mengine, kufunga milango, kuwa na walinzi katika nyumba zetu na kuweka taa za nje tukiamini zinauwezo wa kusaidia upungufu wa uhalifu majumbani mwetu.



Cha kushangaza zaidi, Jitihada hizi binafsi huzioni zikiamishiwa katika udhibiti wa uhalifu huu wa mitandao ambapo vitu kama Antiviruses, Maneno ya siri na mengineyo ni ya kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi.



Kuna Kila namna ya kufahamu kua pale swala la uelewa wa maswala ya usalama mtandao litakapoweza kufanyiwa kazi kwa kiwango kizuri basin i wazi kabisa linaweza kusaidia kila mmoja kuelewa na kuhimili ipasavyo uhalifu huu mtandao katika ngazi ya mtu binafsi, pamoja na kukuza utamaduni wa kila mmoja kujua anajukumu ssi tu la kujilinda binafsi kimtandao bali na kulinda wengine ipasavyo kuhakiki taifa, bara na hatimae dunia inabaki salama kimtandao.



Kwa ufupi nimefafanua kwa kina faida zinazoweza kupatikana pale uelewa sahihi wa elimu ya usalama mtandao itapatikana kwa jamii zetu na katika maofisi yetu (Makampuni) Maelezo hayo yanawea kusomeka kwa ku “BOFYA HAPA” Wakati huo huo nilipozungumzia mambo muhimu yanayo paswa kuenda sambamba na uwepo wa sharia mpya ya usalama mitandao niliainisha kwa kina swala la uelewa sahihi wa maswala ya usalama mitandao pamoja na ujuzi wa kufanyia kazi uchunguzi wa uhalifu mtandao na ushirikiano kama inavyoweza kufatiliwa katika video hii hapo chini.
 


Leo nitaangazia njia ambayo imeshika nafasi ya juu na imeonekana na uwezo mkubwa wa kuhimili uhalifu mtandao ambapo imeaminika inauwezo wa kupunguza aina mbili za wahalifu mtandao pamoja na kusababisha aina ya tatu kupungua makali. Kwa ujumla wake imezungumzwa inaweza kupunguza hadi asilimia 71% ya uhalifu wote mtandao kama itafatwa vizuri na kupewa uzito wa kipekee katika mataifa yote.


Njia hii si nyingine bali ni “Awareness Program” Yaani elimu ya uelewa wa uhalufu mtandao na namna ya kujilinda. Elimu hii inatoa fursa kwa mwananchi wa kawaida kutambua aina mbali mbali za uhalifu mtandao, athari zake, njia ya kujilinda, Na Namna ya kulinda wenzake.

 Natoa wito kwa kila mmoja wetu kukuza upendo wa kufatilia na kutaa kujua namna mbali mbali za kuweza kujilinda katika ngazi ya mtu binafsi na uhalifu huu mitandao unaokua kwa kasi zaidi hivi sasa huku makampuni kua na tamaduni ya kuwa na mafunzo maalum ya maswala haya na taifa kwa ujumla kuhakiki linaongeza jitihada katika kukuza uelewa kwa wananchi katika maswala ya usalma mitandao ili kukabiliana na ongezeko la uhalifu mtandao nchini.
 Na:Yusuph Kileo

Popular Posts

Labels