Thursday, October 1, 2015

KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO ULIMWENGUNI TED N.C.WILSON AJIUNGA NA FACEBOOK NA TWITTER KWA AJILI YA KUWASILIANA NA WAUMINI NA WATU MBALIMBALI



Ted Wilson na mkewe Nancy

Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Ted N.C. Wilson ameziundua rasmi mawasiliano yake kwa njia ya mitandao ya kijamii ya facebook na twitter alhamisi Oktoba 1,mwaka huu ili kuwasiliana moja kwa moja na waumini wa kanisa hilo pamoja na watu mbalimbali.

Wilson anasema atatumia wasifu wake wa twitter kwa anuani yake ambayo ni  @pastortedwilson  na kwenye mtandao wa facebook anatumia ukurasa wake ambao ni facebook.com/pastortedwilson  ambapo atakuwa akiwasiliana na watu kwa njia ya maombi,mafundisho ya Biblia na Roho ya Unabii,taarifa zake za utume,picha na habari mbalimbali za ziara zake za kikazi.

Sikiliza ujumbe wa ukaribisho wa Kiongozi huyo baada ya kujiunga na mitandao hiyo ya kijamii

Mpaka kufikia saa 6:00 usiku wa Alhamisi ya Oktoba 1,2015 tayali watu waliokuwa wameshamfuatilia kwenye twitter ni 1,435 na kwenye ukurasa wake wa facebook kulikuwa na likes 10,050 

Pia kiongozi huyo atatumia ukurasa wake wa facebook kujibu maswali kuhusu kanisa la Waadventista Wa Sabato ambapo watu wataweza kumtumia maswali kupitia anuani yake ya barua pepe ambayo ni e-mail:askpastorwilson@adventist.org na atatoa majibu ya maswali matatu kila ijumaa.

Haifahamiki idadi kamili ya Waadventista Wa Sabato waliko kwenye Twitter na Facebook. Ukurasa wa Facebook wa Divisheni ya Kanisa hilo katika eneo la Kusini mwa Amerika unaonekana kufuatiliwa na watu zaidi ya 877,000 japo hakuna anayafahamu kuwa wote ni Waadventista.

Wasifu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato kwenye Twitter ambao ni  @AdventistChurch,unafuatiliwa na watu  50,300  na kuufanya kuwa unaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi miongoni mwa twitter zinazomiliiwa na makanisa .

Viongozi wengine wa dini walioko kwenye twitter ni Papa Francis ambaye anaidadi ya watu Milioni 25 wanaofuatilia akitumia @Pontifex ambayo inatumia lugha 9 kuwasilia na Dalai Lama ambaye anawatu wanaomfulia milioni 11.9 

Popular Posts

Labels