Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akizungumza kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. |
Kamishina
wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella
Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya
Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl.
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa jumla ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini humo wamepitiwa na mafunzo ya
programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia
teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika
ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa Eusella Bhalalusesa ameeleza hayo wakati akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.
Amesema
kutokana na mafanikio yaliyotokea sasa wanatanua wigo baada ya
kuwezeshwa kifedha na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya elimu (Global
Partnership For Education) kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hiyo
katika kujifunza na kufundisha katika shule za msingi na hasa darasa la
awali la kwanza hadi la nne.
Maonesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere yana lengo la kuonesha ubunifu ambao upo tayari kutumika
kufanikisha mafunzo hayo.
Pia
maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki
zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na
kujifunza kwa gharama nafuu.
Pia wanatarajia kuangalia utayari wa walimu na namna ya kuwabadilisha mtazamo ili waweze kufundisha na kufundishika.
Katika
maonesho hayo serikali imesema inatarajia kuanza kutumia rasmi
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tekinohama) katika kufundishia
wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya elimu ambayo ni chekechea.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
alisema matumizi ya Tehama katika ufundishaji wa wanafunzi wa chekechea
yataimarisha kiwango cha elimu.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa (hayupo pichani).
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akijianda kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali
zinazofanywa na shirika lake katika kuendeleza sekta ya elimu nchini
kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni
Mchome (kushoto) mara baada ya kuzindua maonesho hayo ambapo pia UNESCO
inashiriki. Katikati ni Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa.
Ofisa
anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari
(katikati) akimsikiliza mmoja wa wadau wa elimu aliyetembelea banda la
UNESCO kwenye maonesho ya TEHAMA yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano
wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo.
Ofisa
anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari
(kulia) akiwa na wadau wengine wa elimu wakipitia makbrasha mbalimbali
katika mkutano huo.
Pichani juu na chini ni baadhi wadau wa elimu waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi jijini Dar walioshiriki hafla hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shule Direct, Faraja Nyalandu akipozi na wadau kwenye ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
yanakoendelea maonesho ya TEKINOHAMA