Wizara ya Ulinzi wa Uingereza imetoa Nguo za kisasa kwa ajili ya wanajeshi wake wa miaka ijayo . Picha unayoiona ni mfano wa nguo hizo na huo ni ubunifu wa njia ya kompyuta,mradi huo unaitwa Future Soldier Vision kwa ufupu FSV .
Taarifa zinasema nguo hizo zitakuwa na mfumo wa kisasa wa mawasiliano na mfumo wa biometriki ambao utamfanya mwanajeshi wa Uingereza kuwa salama zaidi kushinda wakati wowote atakapokua kwenye uwanja wa vita .
Katika vita upande wenye taarifa nyingi ndio huwa na uwezekano wa kushinda kwa urahisi . FSV ni mpangilio wa vifaa vya kisasa vya mawasiliano na silaha zinazovaliwa mwilini mwa mwanajeshi . kutakua na sensa itakayowezesha wanajeshi wote kujuana wakiwa uwanja wa vita au kokote bila kuchanganyana , mfumo wa mawasiliano ambao utaweza wanajeshi kutumiana taarifa kwa mfumo wa picha , sauti na video .
Wakati wizara imetoa mchoro huu wa ubunifu na kuuelezea , kampuni , taasisi na watu binafsi wameanza utafiti ambao utawezesha kutengeneza vifaa vingi vitakavyofanya kazi sambamba na wanajeshi hao muda ukifikia kwa ajili ya soko la ndani ya Uingereza na maeneo mengine ulimwenguni.