Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dr Ally Simba |
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), imevitaka vituo vya redio na televisheni nchini Tanzania kuepuka kurusha habari
za uchochezi hasa katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally
Simba ameeleza kuwa vyombo vya habari vinatakiwa kuepuka
kurusha na kuandika habari zitakazochochea vurugu na uvunjifu wa amani kwan jamii
ina imani kubwa na vyombo vya habari na waandishi wa habari, hivyo hawana budi
kutumia weledi katika utoaji wa taarifa katika kipindi hiki cha kampeni
kuelekea uchaguzi mkuu.
Radio 106 na televisheni 28, zimesajiliwa nchini Tanzaia na
kwamba katika kuelekea uchaguzi mkuu, tayari vituo vitano vya televisheni
vimekuwa na makosa yaliyosababisha kupewa adhabu na onyo.