Mkurugenzi
Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Simu katika Wizara ya Ujenzi
,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera akizungumza na wanahabari
katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu jijini Mbeya( TIA ) juu ya zoezi la
uchukuaji maoni na ushauri kwa wadau katika kuboresha sera ya Taifa ya
Habari ,Teknologia na Mawasiliano (TEHAMA).
|
Mhandisi
Enock Mpenzwa Idara Mawasiliano toka Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na
Mawasiliano akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Forest
jijini Mbeya waliofika kwa ajili ya zoezi la utoaji maoni na ushauri juu
ya uboreshaji wa sera mpya ya Taifa ya TEHAMA katika viwanja vya Chuo
Cha Uhasibu TIA jijini Mbeya April 22 ,2015.
|
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Forest jijini Mbeya wakiwa katika
foleni ya kujiandikisha ili kutoa maoni yao na ushauri juu ya
uboreshaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA,zoezi ambalo limefanyika katika
viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Mbeya (TIA) April 22 ,2015.
|
Mwanafunzi
shule ya sekondari Forest jijini Mbeya Mariam Jordan akijiandikisha kwa
ajili ya kutoa maoni yake katika zoezi la uboreshaji wa sera ya Taifa
ya TEHAMA zoezi ambalo limeratibiwa na Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na
Mawasiliano ,katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Jijini Mbeya( TIA)
|
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Jijini (TIA)wakijibu baadhi ya Maswali
kama sehemu ya ukusanyaji maoni ili kuboresha sera ya TEHAMA .
|
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Jijini (TIA) na wadau mbalimbali
kutoka Mkoani Mbeya wakijibu baadhi ya Maswali kama sehemu ya ukusanyaji
maoni ili kuboresha sera ya TEHAMA .
|
Wizara
ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imetoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali
kuendelea kutoa maoni na mapendekezo ili yatumike kuboresha Sera mpya ya Taifa
ya Habari Teknologia ya Mawasiliano(TEHAMA)
ya (2016) ili kuisaidia serikali kutatua changamoto za upatikanaji wa habari na
mawasiliano katika jamii
Wito
huo umetolewa jijini Mbeya na Mkurugenzi
Msaidizi anayeshughulikia maswala ya simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na
Mawasiliano Ndugu John Mwera wakati wa zoezi la uchukuaji maoni lililofanyika
katika viwanja vya chuo cha Uhasibu (TIA) jijini Mbeya .
Amesema Teknolojia ya habari na mawasiliano
hapa nchini imekuwa ikikua kwa kasi kubwa katika kipindi cha miaka kumi tangu
serikali ilipotunga sera kwa mara ya kwanza mwaka 2003.
Amesema hali hiyo imechangia kuwepo kwa miundombinu
ya huduma za mawasiliano kila mahala na kufanya matumizi kuwa makubwa ambapo zaidi
ya watu milioni 39 wanatumia mawasiliano ya simu hivyo kufanya kuibuka kwa
changamoto mbalimbali katika sekta hiyo.
Amesema
ili
kufahamu changamoto wanazo kutananazo wananchi pamoja na mtizamo wao
katika utumiaji wa mawasiliano, wizara hiyo imeamua kuweka utaratibu
wa kuweka
vituo vya kukuza ubunifu katika jamii katika kila mkoa ambapo kila
mwananchi
anakuwa huru katika kutoa maoni yao na ushauri ili kuisaidia serikali
katika
kupanga mikakati ya kuweza kuzitatua changomoto hizo.
“Huwezi
kukaa ofisini ukatunga sera ambazo haziwahusu mwananchi wa kawaida hivyo lazima
twende kwa wananchi na kujua wanahitaji
nini ili kutunga sera na kuweza kuzitatua”Alisema Mwela .
Aidha
amesema kuwa kila maoni yanayotolewa na wananchi serikali inayathamini katika
kuweza kutoa muelekeo wa sekta ya mawasiliano kwani sekta hiyo bado inamchango
mkubwa sana katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.
Hata
hivyo amesema bado wizara inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni elimu ndogo kwa waanchi juu ya
utunzaji wa miundombinu ya sekta ya mawasiliano hususani mkongo wa taifa
sanjali na wizi wa mafuta kwenye minara ya simu hivyo amewataka wananchi kuwa
walinzi wa miundombinu hiyo ili kuendelea kukuza sekta hiyo sanjali na
kulahisisha upatikanaji wa huduma kwa jamii.
Amesema
zoezi hilo la uchukuaji maoni kwa wananchi juu ya uboreshaji wa sera ya TEHAMA
itaendelea inchi nzima katika mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani.