Kanisa la Waadventista Wa Sabato mwaka huu litashiriki mkutano wa Waadventista watalaamu wa mawasilino ya Intaneti duniani (GAiN) kwa kuwakutanisha wataalamu hao kwa njia ya mtandao wa intaneti.
Mkutano huwa wa mwaka ambapo washiriki watakutana kutathimini huduma ya utume kwa kutumia teknojia itakuwa ni februari 11 hadi 15 kupitia tovuti ya gain.adventist.org. na kila mada itawasilishwa na kufuatiwa na mijadala mbalimbali na itatangazwa mara tatu kwa siku ili kuwafikia watu wa kanda mbalimbali duniani.
Waratibu wamesema kuwa wazo la kutumia mtandao ambalo linatazamiwa kuwezesha kupata washiriki wengi kutokana na mikutano mingine ya kanisa inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Kwa mwaka huu mkutano wa wataalamu wa Teknohama utatolewa katika lugha za Kiingereza na kutafsiriwa moja kwa moja kwa Kifaransa,Kireno na Kiispaniola huku wito ukitolewa kwa washiriki kwa makundi kwenye makanisa,ofisini na nyumbani.
Miongoni mwa yatakayojadiliwa ni usalama kwenye mitandao,ubunifu wa program tumishi,elimu masafa,utalaamu wa masoko,utumiaji wa michezo ya komputa kwa injili na uendeshaji wa idara za teknolojia ya habari na mawasiliano kutokana na bajeti.
Waweza jisajili na kuona ratiba ya mkutano huo kupitia gain.adventist.org pia hushtag ya mkutano ni #GAiN15.