Monday, January 5, 2015

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NCHINI TANZANIA YAKIRI MASHINE ZA BVR ZILIZOTUMIKA KWA MAJARIBIO HAZIFAI



Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imekiri kuwa mashine 250 zilizotumika katika zoezi la majaribio la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa kielektroniki (BVR) lililofanyika mwezi uliopita katika majimbo matatu nchini, hazifai.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu tathimini ya utekelezaji wa majaribio ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa BVR.

Jaji Lubuva amesema changamoto zilizojitokeza katika majaribio hayo ambayo yalihusisha watu 41,721 ni pamoja na matatizo ya programu za mifumo ya kompyuta na hali ya hewa ya joto ambayo iliharibu urahisi wa utendaji kazi wa mashine hizo.

Amesema kompyuta mpakato zilizokuwa zikitumika katika kazi hiyo ziliwekewa bati la kuzuia zisiibiwe kwa urahisi lakini iligundulika baadaye kuwa bati hilo lilikuwa likizuia mzunguko wa hewa ndani ya mashine hizo.

Lubuva amesema Zoezi hilo linatarajia kugharimu Shilingi bilioni 293 za kitanzania  ambapo  vitambulisho hivyo ndivyo vitakavyotumika katika upigaji wa kura ya maoni ya Katiba mpya mwezi Machi pamoja na Uchaguzi Mkuu Oktoba.

Katika hotuba yake ya salamu za mwaka mpya wa 2015  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amesema

Moja ya mambo muhimu ambayo Tume ya Uchaguzi inafanya kwa sasa ni kuandikisha wapiga kura katika Daftari la Mpiga Kura. Tume imeamua kutumia mfumo mpya wa Biometric Voters Register. Uandikishaji wa majaribio umefanyika katika baadhi ya Kata katika Majimbo ya Mlele, Kawe na Kilombero. Matatizo yaliyojitokeza yatasaidia kuboresha mfumo huo kabla ya uandikishaji wa watu wote wenye sifa stahiki kuanza.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Moja ya mambo muhimu ambayo Tume ya Uchaguzi inafanya kwa sasa ni kuandikisha wapiga kura katika Daftari la Mpiga Kura. Tume imeamua kutumia mfumo mpya wa Biometric Voters Register. Uandikishaji wa majaribio umefanyika katika baadhi ya Kata katika Majimbo ya Mlele, Kawe na Kilombero. Matatizo yaliyojitokeza yatasaidia kuboresha mfumo huo kabla ya uandikishaji wa watu wote wenye sifa stahiki kuanza.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Tume imeamua kutumia mfumo mpya wa Biometric Voters Register. Uandikishaji wa majaribio umefanyika katika baadhi ya Kata katika Majimbo ya Mlele, Kawe na Kilombero. Matatizo yaliyojitokeza yatasaidia kuboresha mfumo huo kabla ya uandikishaji wa watu wote wenye sifa stahiki kuanza.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_wi


Tume imeamua kutumia mfumo mpya wa Biometric Voters Register na uandikishajiwa majaribio umefanyika katika baadhi ya Kata katika Majimbo ya Mlele, Kawe na Kilombero na kuleeza kuwa matatizo yaliyojitokeza yatasaidia kuboresha mfumo huo kabla ya uandikishaji wa watu wote wenye sifa stahiki kuanza.
Napenda kutumia nafasi hii kuwafahamisha Watanzania wenzangu wote kuwa mfumo mpya unatengeneza Daftari Jipya la Mpiga Kura ingawaje lugha inayotumika ni uboreshaji wa Daftari la sasa. Uboreshaji huu wa Daftari la Mpiga Kura ni tofauti na ule tuliouzoea ambapo walikuwa wanaandikishwa wapiga kura wapya na wale waliopoteza vitambulisho vyao. Safari hii wanaandikishwa wote wapya na wa zamani na wote watapata vitambulisho vipya. Hivyo basi, sisi wenye vitambulisho vya kupiga kura vya zamani tusifanye ajizi, tujitokeze kujiandikisha wakati ukifika.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_wi




Popular Posts

Labels