Mfumo endeshi wa Android katika vifaa vya mawasiliano hasa simu ni miongoni mwa mifumo inayoonekana kufanya vyema na kutumiwa sana duniani kwa sasa.
Android ulioanzishwa ulivumbuliwa na Andy Rubin, Rich Miner, Nick Sears na Chris White huko Palo Alto, California,Marekani walianzia mbali katika maendeleo yake.
Walikuwa wanalengo la kutengeneza programu za komputa kwa ajili ya kamera lakini baada ya kugundua kuwa kamera hazina soko kubwa waliamua kuanzisha kwa siri mfumo wa Android ili waweze kushindana na mifumo endeshi ya Symbiani na windows
Agosti 17,2005 kampuni ya Google ilihitaji japo waanzilishi hawa hawakufahamu kama kampuni hiyo ya mawasiliano ya intaneti itaweza kuingia katika soko la simu za mikononi kwa hapa ilipofikia.
Toka mwaka 2008, Android imekuwa ikitoa na kufahamika kwa matoleo yake ambayo ni Alpha 1.0, Beta 1.1, Cupcake 1.5, Donut 1.6, Éclair 2.0 – 2.1, Froyo 2.2 – 2.2.3, Gingerbread 2.3 – 2.3.7, Honeycomb 3.0 – 3.2.6, Ice Cream Sandwich 4.0 – 4.3.1, Jelly Bean 4.1 – 4.3.1, Kitkat 4.4 – 4.4.4 na Lollipop 5.0 – 5.0.2