Mchungaji Lusekelo Mwakalindile akizungumza toja jijini Dar es salaam na wajumbe waliohudhuria mkutano wa mawasiliano uliofanyika Njiro Arusha kwa kutumia skype |
Viongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania katika
idara ya mawasiliano wameaswa kubuni na mikakati ya kuwaelekeza
washiriki namna sahihi ya utumiaji bora wa mawasiliano ikijumuisha mitandao ili
kazi ya injili iende kwa kasi zaidi.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Mawasiliano kanda ya Afrika
mashariki na Kati Mchungaji,Steven Bina katika ufungunzi wa kikao cha idara ya
mawasiliano katika Unioni Konferensi ya kaskazini mwa Tanzania kilichofanyika Njiro
jijini Arusha kwasiku nne.
Aidha Mchungaji bina,amesema kuwa idara ya mawasiliano ndio
idara inayounganisha idara zingine hivyo haina budi kuweka njia mbalimbali zinazoweza kuwaelekeza washiriki na wasio washiriki namna sahihi ya kutumia
vyombo vya habari vya kanisa ili waone umuhimu wa vyombo hivyo ndani na nje ya
kanisa.
Mkutano huo uliwahusisha
viongozi kutoka konferensi nne za union hiyo ambazo ni konferensi ya kusini mwa Tanzania,konferensi ya kaskazini mwa Tanzania,konference ya magharibi mwa Tanzania pamoja na konferensi ya mara.
Wajumbe wa mkutano huo pia walifanya mazungumzo maalum ya Kimtandao kupitia kupitia mtandao wa kijamii wa Skype
na Morning Star Radio na Tv kupitia wakurugenzi wa vituo hivyo vilivyoko
jijini Dar es salaam, Ndugu Mazara Matucha wa Tv na Mchungaji Lusekelo
Mwakalindile wa Radio,hii ikiwa ni katika kuboresha na kutatua changamoto
zinazovikabili vyombo vya habari vya Kanisa hilo nchini.