Wakati ugonjwa wa Ebola ukiendelea kuwa tishio katika baadhi
ya nchi za Afrika magharibi, Wataalam wa afya nao wameendelea kuweka jitihada
zaidi kuhakikisha kuwa wanaumaliza ugonjwa huo.
Katika jitihada zao hivi sasa wamebuni mpango wa mawasiliano
ya simu ya mkononi wenye programu maalum inayotoa taarifa kutoka maeneo
yaliyokumbwa na Ebola.
Programu hii ya simu imesambazwa katika maeneo mbalimbali
nchini Guinea ambapo ugonjwa huu umesambaa kwa kiasi kikubwa, programu hii
huweza kuonesha maeneo ambayo yako hatarini kuathiriwa naVirusi vya Ebola.
Shirika linaloshughulikia idadi ya Watu duniani, UNFPA
linatoa elimu kwa wafanyakazi wa jumuia kuhusu namna ya kutumia programu hiyo
inayowezesha kushirikisha taarifa kwa kwa wataalamu wa afya katika ngazi ya
kitaifa na kimataifa.
Zaidi ya Watu 1,700 wamepoteza maisha nchini Guinea kutokana
na Ebola