Saturday, September 5, 2015
SAMSUNG NA MIT KUTENGENEZA BETRI ZA SIMU ZINAZOTUNZA NISHATI YA UMEME KWA MUDA MREFU
Huenda umekuwa ukikumbana na tatizo la betri za simu hizi za kisasa kuisha nguvu yake ya nishati ya umeme mapema yaani kuisha chaji,watumiaji wengi wanadai kuwa simu za kisasa kuwa na program tumishi nyingi zinazfanyakazi kwa wakati mmoja yaweza kuwa ni sababu ya kuisha kwa betri katika simu za kisasa.
Tatizo hili huenda likapata ufumbuzi kwa sababu kampuni ya simu ya Samsung kwa kushirikiana na Taasisi ya Teknolojia Massachusetts (MIT) wameanza mpango mkakati wa kutengeneza betri za simu zisizokwisha uwezo wake wa kutoa nishati ya umeme katika simu.
Pia watafiti wanaendelea na utafiti utakaowezesha kuchaji simu za kisasa kwa kutumia teknolojia ya WiFi.
Kwa kawaida betri ya simu imeundwa kwa vitu vitatu moja ni kimiminika kiitwacho electrolyte,wanasayansi wamegundua njia ambayo itasaidia kuunda betri iinayotumika muda mrefu kwa kutengeneza electrolyte ambayo haiko katika hali ya kimiminika.
Njia itasaidia kuondoa tatizo la betri kuisha chaji na kuzimika kwa simu.