Saturday, September 5, 2015

PROGRAM TUMISHI YA KUPAMBANA NA UBAKAJI KUZINDULIWA NCHINI DRC MWAKA UJAO



MediCapt App

Shirika la kujiolea la nchini Marekani linalojihusisha na utabibu na masuala ya haki za binadamu (PHR) limetengeneza program tumishi mpya ambayo itawasaidia kupata haki za kisheria  watu waliothirika na ubakaji huko Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).

Umuhimu wa kutengenezwa program tumishi hiyo ulianza kuonekana mwaka 2011 baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kuonesha kuwa  wastani wa wanawake 48 walibakwa kila baada ya saa moja kati ya mwaka 2006 na 2007 .

Taarifa hiyo inaonesha kuwa maeneo ya vijijini huko DRC  yamekuwa yakishikiliwa na waasi ambapo waasi hao wakati mwingine wamekuwa wakichoma nyumba,kuwachukua watoto na kuwabaka wanawake.
Kutokana na hali hiyo kumekuwa na tatizo la ukusanyaji na upatikanaji wa taarifa za matukio hayo ya kuwadhalilisha watoto na wanawake katika maeneo hayo yanayokaliwa na waasi nchini humo.

PHR imekubali kushirikiana na umoja wa mataifa  na hivyo imetengeneza program tumishi iitwayo MediCapt.Ni program tumishi ambayo itakuwa na uwezo wa kupeleleza na kutunza taarifa za udhalilishaji huo na kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya kuhusu uharifu huo wanaofanyiwa wanawake nchini humo tofauti na awali ambapo walikuwa wakitumia taaarifa za kuuliza tu.

Program tumishi hiyo itakuwa na uwezo wa kupiga picha na kuhifadhi taarifa za tukio hata kama hakuna  na mtandao wa intaneti na kutuma taarifa hizo katika kituo cha kukusanya data.Kwa sasa tayali wataalamu wa teknohama watakaoratibu program tumishi hiyo inayotumika kwa simu zenye mfumo endeshi wa androd wako nchini DRC katika kuhakikisha inaanza kutumika mapema mwakani.

Popular Posts

Labels