Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania
(TCRA) Dr. Ally Yahaya Simba(Pichani),amesema pamoja na mafanikio katika sekta ya
mawasiliano nchini Tanzania lakini bado kuna matatizo yanayojitokeza ikiwemo ukiukwaji
wa kwa sheria za mawasiliano.
Ameyasema hayo jijini Arusha alipofanya ziara yake
fupi ya utambulisho katika kanda ya kaskazini huku kaiwataka wadau wa
mawasiliano na vyombo vya Habari nchini kumpa ushirikiano ili kuboresha sekta
hiyo katika kipindi cha uongozi wake.
Dr. Ally Simba amesema pamoja mafanikio yaliyopo
katika sekta ya Mawasiliano nchini lakini bado kuna matatizo yanayojitokea kutokana na
watumiaji wa huduma ya mawasiliano ikiwemo ukiukwaji wa masharti ya leseni na
matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
Aidha amewapongeza wadau wa Mawasiliano na vyombo vya
habari kwa kuzingatia sheria na kanuni za utoaji wa Habari na utangazaji katika
msimu huu wa kampeni za uchaguzi mkuu.