Friday, September 18, 2015

NDEGE MAALUM ZISIZO NA RUBANI SASA KUTUMIKA KUPAMBA NA UJANGILI NCHINI TANZANIA

Ndege isiyotumia rubani aina ya Super Bat DA-50 katika majaribio.Ndege hii na nyingine nyingi zitatumika katika kuimarisha vita dhidi ya ujangili nchini.Zitakuwa zinaruka katika maeneo mbalimbali ya Mbuga za wanyama,misitu na meeneo mengine kuimarisha usalama wa wanyama

 
 


Natumaini umeshasikia kuhusu ndege ambazo hazina rubani maarufu kama drones.

Kwa siku za karibuni zimekuwa maarufu kwani zinatumika kupeleka misaada mbalimbali hata katika maeneo hatari ya vita ambako hakufikiki kirahisi.


Nchini Tanzania tumeanza kuitumia teknoloia hii yanaweza kuwa maendeleo mengine mapya.

 Phil Jones ni ofisa mwendeshaji wa mitambo  kutoka kampuni ya MartinUAV ya Marekani iliyotengeneza ndege hiyo aina ya Super Bat DA-50 UAV 

Ndege hiyo  haihitaji kuwa na rubani, inaongozwa kwa kompyuta maalum, ina antenna mbili, ina kamera maalum ambazo zinaweza kupiga picha usiku na hata mchana.

Akasema ndege hiyo ina uwezo wa kuruka urefu wa futi 20,000 kutoka usawa wa bahari na kwenda katika nusu kipenyo cha kilometa 35 kutoka ilipo mitambo ya kuiongoza.

Jones, ambaye ni rubani wa zamani wa ndege za kijeshi katika Jeshi la Uingereza aliyestaafu mwaka 2014 ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, anasema ndege hiyo inayorushwa kwa mtindo wa manati (catapult launch system), inaweza kuruka mfululizo kwa muda wa saa 10 ikiwa angani kabla ya kutua na kujazwa mafuta tena hivyo ni rahisi kubaini kama kuna majangili.


Ndege hii inatua kama ndege za kawaida , tofauti yake tu yenyewe haina magurudumu. Naam, unaweza kuwa ufumbuzi mwingine wa kupambana na ujangili nchini, tatizo ambalo haliko Tanzania tu, bali katika nchi nyingi barani Afrika.


Taasisi mbalimbali za ndani na nje zikiwemo serikali za mataifa makubwa zimekuwa zikijitahidi kusaidia mapambano hayo kama alivyofanya Rais Barack Obama wa Marekani alipoahidi kutoa Dola milioni 10 (sawa za Shs. 20 bilioni) ili kuimarisha mapambano hayo nchini.


Takwimu zinaonyesha kuwa Bara la Afrika mwaka 1930 lilikuwa na tembo 50 milioni na kwamba hadi kufikia mwaka 2013 tembo waliobakia katika bara zima ni  500,000.

Popular Posts

Labels