Baada ya kuwepo kwa uvumi wa kipindi kirefu kuwa kampuni ya Apple inampango wa kutengeneza magari yake hatimaye siri zimeanza
kuvuja.
Kulingana na ripotI iliyochapishwa katika tovuti ya The Wall Street Journal, vyanzo
vya kuaminika kutoka kampuni hiyo inayofanya vizuri katika vifaa vya
teknolojia za mawasilianio na elektroniki, vimesema kuwa kampuni hiyo
itaanza kuuza magari yake yanayotumia nishati ya umeme ifikapo mwaka 2019.
Licha ya kuwepo na kampuni nyingine nyingi kama Tesla
ambazo tayari zinatengeneza magari yanayotumia nishati ya umeme, Apple imedhamiria kujiingiza katika biashara hiyo.
Je, wataleta mapinduzi yoyote kama yale waliyo fanya katika Kompyuta na simu za kiganjani?
Chanzo:http://www.classicnewstz.com