Kampuni ya Microsoft
imesema kuwa watumiaji wa program za kompyuta, wanapaswa kutumia program zenye
viwango na kujiepusha na zisizo na viwango.
Akizungumza hii leo katika
mkutano wa matumizi ya program za kompyuta,Afisa mtendaji na
msimamizi wa Hakimiliki wa COSOTA, Dorine Sinare amesema kuwa, kutumia program za
kompyuta zilizo bora zitasaidia kuepuka uharamia katika mitandao na serikali
kuweza kuongeza mapato yaliyotokana na program hizo.
Dorine amesema kuwa wameanza
kushirikiana na Microsoft katika kuweza kutoa elimu juu ya matumizi ya program
ambazo halisi na kuachana na ambazo si halisi kwani zinaweza kuharibu program
zingine.
Njiru ameongeza kuwa Microsoft
inafanya kazi katika kuhakikisha watu wanapata mawasiliano yenye kiwango
kutokana na utoaji wa huduma za program za komputa zenye kiwango.