Thursday, November 3, 2016
TTCL NA HUAWEI WAZINDUA MTANDAO WA 4.5 G
Kampuni ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Huawei Tanzania na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) zimeungana na kuzindua mtandao wa 4.5 utakaokuwa wa kwanza kwa mitandao yote nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bruce Zhang amesema uzinduzi huo unadhihirisha mafanikio ya TTCL kwenye safari ya mabadiliko ya kukua kibiashara nchini.
Hivi karibuni serikali ya Tanzania ilitangaza kumiliki hisa zote za TTCL baada ya kuchukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Bhart Aitel.