Kampuni
Maarufu ya KAGOYA ya Nchini Japan Imeshambuliwa kimtandao ambapo taarifa
binafsi na za kibenki za wateja wake zimedukuliwa.
Uhalifu
huu umegundulika mwezi huu (Desemba, 2016) na tayari kampuni husika imesha toa
taarifa kwenye vyombo vya usalama vya Nchini humo - Ambavyo pia vimeanza
uchunguzi rasmi.
Kampuni
hiyo imesema, Wateja wake waliotumia "Credit card " zao baina ya Aprili
Mosi , 2015 hadi september 21, 2016 wameathiriwa na uhalifu huu na imewaasa
wateja wake wafatilie taarifa za utoaji pesa wa kadi zao.
Mjumuiko wa taarifa zilizo ibiwa ni, majina , barua pepe, Namba za simu, Namba za kadi za benki, maneno ya siri (Nywila) pamoja na taarifa nyingine za wateja wake.
Hii
si mara ya kwanza kwa Nchi ya JAPANI kupata shambulio kubwa la kimtandao kwa
mwaka huu (2016) pekee - Itakumbukwa, Mwezi May mwaka huu (2016) zaidi ya Yuan
Bil. 1.5 sawa na Dola Milioni 13 ziliibiwa katika ATM zaidi ya 1400 ndani ya
masaa mawili na nusu.
Aidha,
TANZANIA hali ya uhalifu mtandao bado ni changamoto inayo hitaji suluhu ya
kudumu. Kuibiwa kwa Fedha na Taarifa , Matumizi mabaya ya mitandao, Tovuti
kudukuliwa ni miongoni mwa matukio yaliyo jitokeza kwa mwaka huu 2016.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi Bodi ya TCRA (Mamlaka ya Mawasiliani Tanzania) Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya TCRA, kuhakikisha
wanapata mwarobaini wa kudhibiti ongezeko la wizi wa mitandao unaoendelea
kukithiri hapa nchini.
Prof.
Mbarawa amesema watanzania wameibiwa kwa muda mrefu kupitia njia ya ujumbe
mfupi na kushawishiwa kutoa fedha kwa njia ya udanganyifu na hivyo kuitaka bodi
hiyo kutofumbia macho changamoto hiyo.
“Changamoto
ya wizi wa mitandao inagusa watanzania wengi, mkiwa na jukumu la kudhibiti mna
wajibu wa kuwalinda wananchi”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa bodi hiyo ihakikishe inasimamia kwa karibu sheria, kanuni na taratibu
zilizowekwa katika kudhibiti ubora wa masuala ya mawasiliano ikiwa ni
teknolojia inayokuwa kwa kasi kubwa.
Aidha
Prof. Mbarawa ameitaka bodi hiyo kuendelea kudhibiti wimbi la meseji za
uchozezi zinazotumwa na baadhi ya wananchi kwa kukosa maadili.
Katika
kuimarisha huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Waziri Prof.
Mbarawa ameikata TCRA kufanya maamuzi ya haraka na kuwa wabunifu ili kuweka
mazingira endelevu ya kukuza sekta hiyo.
Aidha,
Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TCRA Dkt. Jones Kilimbe amesema kuwa pamoja na
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo, Bodi itahakikisha inapata
suluhu ya changamoto hizo ndani ya muda mfupi.
Hatuna
Budi kutambua kua janga la uhalifu mtandao ni kubwa na athari zake zimekua
zikionekana situ kwa nchi zisizo na teknolojia nzuri ya kukabiliana na uhalifu
mtao bali pia Nchi zilizo endelea zimekua wahanga wa janga hili.
Taifa
la Tanzania halina budi bali kuanza na utayari uliombatana na kujipanga upya na
vizuri kukabiliana na Wimbi la uhalifu mtandao nchini.
Changamoto
za urasimu, matumizi makubwa ya pesa kwenye kampeni za kukuza uelewa zinazokosa
matokeo chanya pamoja na kutojiongezea elimu ya mara kwa mara ya kukabiliana na
uhalifu huu mtandao lazima ipaiwe suluhu.
Sheria
Mtandao pekee haziwezi kutuvusha kwenye wimbi hili la ukuaji wa uhalifu mtandao
nchini, Lazima mambo mengine muhimu ya kukabiliana na uhalifu mtandao yafanyiwe
kazi.
Naziasa
taasisi binasfi na za serikali kujenga tabia ya kutoa taarifa ya matukio ya
kishambulizi mtandao mara tu yanapo gundulika ili iwe rahisi kupatiwa suluhu.
Bila kufanya hivyo wahalifu mtandao wataendelea kupata nguvu.
Kwa
sasa Tanzania, Hatujafikia pabaya sana kulinganisha na mataifa mengine – Ila,
Kama hatua za haraka na za dhati za kujipanga na kufunga mikanda
hazitachukuliwa mapema, Mbele yetu ni mbaya Mno.
Na:Yusuph Kileo