Kampuni ya Intaneti ya Yahoo inasema wavamizi wa mitandao waliiba data za zaidi ya ya watumiaji wake bilioni moja. Tukio hilo linaaminika kufanyika mnano mwaka 2013.
Katika taarifa yake, Yahoo inasema uvamizi huo wa taarifa muhimu ni
tofauti na ule ulioripotiwa mwezi Septemba mwaka huu, ambapo wavamizi
hao waliiba taarifa kutoka kwenye akaunti mbalimbali za watumiaji zaidi
ya milioni mia tano.
Imeongeza kuwa data zilizoibiwa zinajumuisha majina, anuani, namba za simu,tarehe za kuzaliwa pamoja na nywila (namba za siri).
Lakini kadi za malipo sambamba na akaunti za benki hazikuingiliwa.