Baadhi ya Wataalamu wa Teknohama wa Taasis za Kanisa la Waadventista |
Wataalamu wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato
wametakiwa kutumia utaalamu wao katika masuala ya usalama kwenye mtandao,ubunifu
wa program tumishi na program za komputa za utambuzi wa maeneo katika
kufanikisha utume duniani.
Akitoa mada
kwenye mkutano wa wataalamu wa intaneti wa kanisa la waadventista duniani (GAiN)
ulioanza Februari 11 mwaka huu unaofanyika kwa njia ya mtandao na unaoratibiwa toka Marekani yalipo makao makuu
ya kanisa hilo na kuwakutanisha washiriki
toka nchi 70 duniani Mkurugenzi wa Teknohama wa Divisheni ya Marekani ya
Kaskazini David Greene amewaasa wanateknohama kuhakikisha tovuti wanazosimamia
na kuzitumia zina ulinzi wa kutosha.
Greene amesema
kuwa asilimia 80 ya usalama wa tovuti
utakuwa umeondoka baada ya miaka miwili
na hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha kuongeza usalama huo,na amewahimiza
wataalamu wa tovuti za kanisa kuhakikisha wanapata vikoa vyenye usajili rasmi
na vinavyotambuliwa kisheria.
Mkutano wa GAiN
utamalizika February 15,huku mada na
mijadala mbalimbali ya teknohama
ikifanyika mara tatu kwa siku kwa
ajili ya kuwafikia washiriki walioko kwenye maeneo mbalimbali duniani ambapo
unaweza kushiriki kwa kutembea katika tovuti ya gain.adventist.org na mada
zilizojadiliwa zitawekwa baada ya majuma kadhaa ya mkutano huo.