Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha
Kazaura (kushoto) na Ofisa Ufundi (IT) wa kampuni hiyo, Rehema Maswanya
(kulia) kwa pamoja wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa teknolojia ya
4G LTE iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Kampuni
ya Simu nchini Tanzania (TTCL) imezinduwa mtandao unaotumia
teknolojia ya 4G LTE unaoanza kutoa huduma jijini Dar es Salaam. Mtandao
huo wenye teknolojia mpya na ya kisasa wenye kasi kubwa utatoa huduma
katika maeneo 11 ambayo ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K.
Nyerere, Pugu Road, Posta Mpya, Upanga, Kinondoni, Ubungo, Oysterbay,
Mwenge, Mbezi Tangibovu, Mbezi Exchange, Kunduchi Salasala, na Wazi
Tegeta.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akizinduwa rasmi teknolojia hiyo, Ofisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema licha ya kuzinduwa
huduma hiyo katika maeneo 11 kwa sasa mafundi wa kampuni hiyo wapo
kazini wakiendelea na awamu ya pili ya kufunga mitambo ili huduma hiyo
itolewe pia katika maeneo mengine 14 ya jiji la Dar es Salaam.
Aliyataja
maeneo mengine ambayo mitambo inaendelea kufungwa kwa sasa kuwa ni
pamoja na Kigamboni, Masaki, Temeke, Kimara, Jangwani, Kariakoo, Chuo
Kikuu, Kurasini, Mbezi Chini Gongo la Mboto, Tabata, Kibamba, Kongowe na
Bunju.