Jeshi la Polisi mkoani Arusha na Kampuni za Ulinzi wameweka mkakati wa kushirikiana katika kupeana taarifa za uhalifu kwa kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.
Mpango huo umetangazwa na Mkuu wa Operation wa Jeshi la Polisi Arusha Edward Balele ambapo amesema awali taarifa zilikuwa zikiwafikia walengwa kwa mtindo wa ujumbe mfupi (SMS) lakini kwa kutumia mfumo wa kikundi cha WhatsApp ambacho kitapewa jina maalum,taasisi hizo zitakuwa zinapata na kutoa taarifa kwa pamoja ambapo kila mhusika atakuwa anachingia mawazo yake huku wanawachama wengine wa kikundi hicho wakiona maoni ama ushauri wa kila mchangiaji.