Friday, September 19, 2014

TEKNOLOJIA YA HUDUMA ZA KIBENKI KUPITIA M-PESA YAANZA KUTUMIKA ULAYA


The M-Pesa mobile money transfer system allows clients to send cash with their telephones (Reuters)
Picha kwa Hisani ya (Reuters)
 
Kwa muda mrefu nchi za Afrika zimekuwa zikitegemea teknolojia zilizobuniwa na kuundwa kutoka nje ya bara hilo,Kwa sasa teknolojia ya huduma za kibenki kupitia simu za mkononi iliyobuniwa na kuanza kutumika nchini humo imeanza kutumiwa barani Ulaya.

Teknolojia ya Huduma za kibenki kwa kutumia simu za mkononi ya M-Pesa ambayo inampatia nafasi mteja kutuma pesa kupitia simu mkononi imeonesha namna biashara inavyofanyika katika nchi za Afrika Mashariki na sasa imeanza kushika kasi katika matumizi yake nchini Romania.

Afisa wa Kampuni ya Vodafone nchini Kenya ameliambia shirika la Habari la AFP  hivi karibuni jijini Nairobi kuwa nchin zingine duniani zinapaswa kutazama matumizi ya huduma za M-Pesa kwani kuna mambo ambayo yanaweza kuchukuliwa toka nchi zinazoendelea na kupelekwa katika nchi zilizoendelea.

Huduma ya M-Pesa  ilianza kutumika  nchini Kenya mwaka 2007 na kampuni ya mtandao  wa simu ya  Safaricom ambayo ni kampuni ya simu kubwa nchini humo yenye ushirikiano wa kibiashara  na kampuni ya simu ya Vodafone ya nchini Uingereza ,

Nchini Kenya huduma ya M-Pesa imekuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ikiwa na wateja milioni 18 ikitumiwa na therusi mbili ya wakazi wa nchi hiyo huku ikihusisha mzunguko wa zaidi ya milioni 8 kwa siku.

Huduma hii huhusisha njia za kibenki kwa kutumia program tumishi inayopatikana kwa urahisi kwenye  simu za mkononi kwa kufanya malipo ama manunuzi ya bidhaa mbalilimbali au kutuma pesa kwa jamaa,ndugu,marafiki na wazazi.

Romania ni nchi ambako kampuni ya Vodafone imenza kuwekeza katika huduma zake za M-Pesa ikiwa ni nchi ya kwanza toka huduma hiyo ianze nchini humo mwezi machi mwaka huu ikihusisha malipo kwa njia ya mtandao wa intaneti.

Michi Carstoiu,mhandisi toka mji mkuu wa Romania  Bucharest anasema huduma hiyo ni nzuri inaokoa muda na inatozwa gharama kidogo kwa mtumiaji

Barani Afrika huduma ya M-Pesa kwa sasa inatumia  Misri,Lesotho,Msumbiji na Tanzania na imeanzishwa hivi karibuni nchini India.


DEREVA ATAKAYE KAMATWA AKIENDESHA GARI HUKU AKIONGEA NA SIMU KUFUTIWA LESENI

Picha kwa hisani yan http://www.sligotoday.ie
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani nchini Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri wa Nchi kavu na Majini SUMATRA limeanzisha mkakati wa kuwafungia leseni madereva watakaobanika kuendesha magari huku wakiwa manazungumza na simu za mkononi.

Zoezi hilo limekuja kufuatia kile kinachodaiwa kuwepo kwa ongezeko la ajali za barabarani ambazo zinasababishwa na uzembe ambao unasababishwa na unywaji wa pombe,kuchoka na kuzungumza na simu hizo.

Takwimu zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio 264 ya ajali barabarani kwa mwaka 2013 sawa na asilimia 1.1 tofauti na mwaka 2012 ambapo matukio yalikuwa 23,578.

Kwa mwaka huu kati ya januari hadi June idadi ya ajali zilizoripotiwa zilikiwa 8,405 zilizosababisha vifo 1743 na majeruhi 7,523 hali ambayo Kamanda Mpinga anasema ipo mikakati mbadala ya kukabiliana na hali hiyo.

Inatajwa kuwa madereva wengi hawana tabia ya kupima afya zao mara kwa mara,inaelezwa kuwa magonjwa ya macho,kisukari pamoja na shinikizo la damu pia linachangia ajali nyingi.

WATUMISHI WA UMMA NCHINI TANZANIA KULIPWA MISHAHARA KUPITIA AKAUNTI ZAO ZA BENKI

Serikali ya Tanzania imeagiza watumishi wote wa umma walipwe mishahara moja kwa moja kupitia akaunti zao sahihi za benki ambazo zitatumika kupitishia mihahara yao.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha nchini Tanzania Mwigulu Nchemba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisi za Hazina jana jijini Dar es salaam.“Mishahara ya Watumishi wote wa Serikali, wakala na taasisi za umma italipwa moja kwa moja kupitia akaunti zao za benki” alisema Mwigulu.

Ili kufanikisha adhima hiyo ya Serikali ya Tanzania, Mwigulu aliwaagiza waajiri wote wa sekta ya umma kuwa wawe na akaunti namba za benki za watumishi wao wote waliochini ya fungu husika ambazo zina taarifa sahihi na wakizingatia mfumo sahihi wa taarifa za kiutumishi.

Mwigulu alionya kuwa mtumishi asiye na akaunti benki asilipwe mshahara wake dirishani ambapo amewahimiza waajiri kuwasisitiza watumishi walio chini yao kufungua akaunti sahihi ya benki kwenye mfumo ambayo itatumika kulipa mshahara husika kupitia orodha ya malipo ya mshahara (payroll) inayotolewa na Hazina.

Aidha, Mwigulu amasema kuwa kila ifikapo tarehe 10 ya kila mwezi waajiri wote wawe wamewasilisha maombi ya fedha za kulipa mishahara kwa mwezi unaohusika wakiambatisha orodha ya malipo ya watumishi ya kuthibitisha kiasi kinachoombwa.

“Waajiri watakaoshindwa kutoa ‘Payroll’ watasababisha watumishi wanaowaongoza kushindwa kupata mishahara yao kwa mwezi husika jambo ambalo sio nia ya Serikali” alisisitiza Mwigulu.

Utaratibu huu wa kulipa mishahara utakuwa endelevu na umedhihirisha kuwa na tija kwa matumizi ya fedha za umma kwani umeonesha mafanikio ambayo kwa mwezi wa saba na wa nane hakuna mtumishi, Wakala za Serikali wala Taasisi iliyolalamika kukosa mishahara.

Eleuteri Mangi-MAELEZO

Tuesday, September 9, 2014

MAREKANI YAJIUNGA NA MUUNGANIKO WA KIMATAIFA WA MAPAMBANO DHIDI YA UHALIFU MTANDAO

 
Maswala ya udukuzi yameendelea kushika kasi katika maeneo mbali mbali ulimwenguni ambapo mataifa mbali mbali yameamua kuunganisha nguvu ya pamoja kupambana na uhalifu mtandao.Kuna umuhimu wa kupata chombo kimoja chenye jukumu la kupambana na uhalifu mtandao ambacho kitatoa nguvu kubwa ili kuweza kukabiliana na hali mbaya ya uhalifu mtandao hivi sasa.
 
Kundi jipya lenye makao yake barani ulaya linalounganisha pamoja nchi wanachama wa bara ulaya pamoja na Canada, Colombia, Australia na marekani limedhamiria kuunganisha mataifa mengine na kuhakiki maswala mbali mbali yahusuyo usalama mtandao yanafanyiwa kazi ipasavyo.

Kwa wafatiliaji wa habari za maswala ya usalama mitandao watakua wamepata  kuona taarifa mbali mbali za hivi karibuni zenye kuonyesha ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao ambapo umetabiriwa kushika kasi zaidi kadri muda unavyo zidi kwenda ambapo uhalifu mwingi wa sasa unategemewa kuhamia katika mitandao.
Katika andiko la naibu mkurugenzi wa chombo cha uingereza kinacho shughulikia maswala ya uhalifu mtandao pamoja na kiongozi  wa kundi jipya la muunganiko wa nchi la kukabiliana na uhalifu mtandao wame elezea ukuaji wa changamoto mbali mbali kwa vyombo vya usalama katika mataifa mengi na kusisitiza kuna umuhimu mkubwa wa kuunganisha nguvu za pamoja ili kuweza kufanikiwa katika vita dhidi ya uhalifu mtandao.

J-CAT imedhamiria kuzileta pamoja nchi wanachama pamoja na mataifa mengine yatakayo onyesha utayari ili kuweza kukabiliana kwa pamoja dhidi ya uhalifu mtandao ambapo matumaini makubwa yatakua ni kukusanya taarifa za kiuhalifu kutoka katika makampuni ya serikali na binafsi ili kubaini aina za uhalifu na kujua maeneo athirika zaidi ili kuweza kuunganisha nguvu. Nchi zaidi zitaenelea kushirikishwa baada ya majaribio ya mpango huu wa kuunganisha nguvu kuweza kufikia pazuri.

Chombo cha upelelezi cha Marekani (FBI) kimebainisha kulipa kipaumbele cha juu swala la mapambano dhidi ya uhalifu mtandao kutokana na kilicho zungumzwa na mkurugenzi wake ya kuwa nchi hiyo tayari imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na wahalifu wanao onekana na kwa sasa wahalifu mtandao kua ndio changamoto yake kubwa na hivyo wameazimia kuanza mapambano na uhalifu huo.
 
 
Kwa upande mwingine katika mkutano mkuu wa maswala ya usalama mtandao wa mwisho wa mwaka ambapo nimeteuliwa kuwa katika panel ya washauri mada zinazotegemewa kujadiliwa na wataalam kutoka maeneo yote duniani ni pamoja na kutafuta njia rafiki ya kufikiwa kwa malengo ya kuunganisha hasa bara la afrika kuweza kuwa na njia ya pamoja ya kupambana na uhalifu mtandao huku maswala ya kisheria  za kimtandao yanavyo sumbua mataifa mbali mbali nini utatuzi wake. 

Panategemewa kupatikana taarifa kamili ya mkutano huo mapema ili watanzania ( wenye ufahamu wa maswala ya usalama mtandao) nao waweze kushiriki.
Na:Yusuph Kileo


Wednesday, September 3, 2014

WIZARA YASEMA MKONGO WA TAIFA UMESAIDIA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAWASILIANO TANZANIA



Wizara ya mawasiliano  sayansi na teknolojia imesema mkongo wa mawasiliano nchini Tanzania umefanikiwa kupunguza gharama za mawasiliano kwa watumiaji wachini ktk maeneo ambayo makampuni ya simu yameshindwa kuyafikia.

Akizungumza na waandishi wa habarI jijini Dar es salaam msemaji mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi amesema mkongo huo unasaidia jamii ambapo huduma zinazohitaji viwango vikubwa vya njia ya mawasiliano kama Elimu Mtandao, Biashara Mtandao, Afya mtandao, mikutano mtandao zinapatikana kupitia mkongo huo.

Bi Ulomi amesema mkongo huo umejengwa kwa viwango vya hali ya juu vya kimataifa na kuongeza kuwa kupitia kifaa hicho Tanzania imekuza mahusiano nanchi jirani za Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi ,Uganda na Kenya kwani makampuni ya simu nchini Tanzania yametumia mkongo huo kuunganisha nchi hizo.

Ameongeza kuwa mkongo huo wa kimataifa ulioenea ktk maeneo mengi hapa nchini pamoja na nchi jirani ktk awamu ya kwanzana ya pili utasaidia kufikisha huduma kwa wananchi kwa unafuu na kuhakikisha maendeleo ya taifa kwani wananchi watapata fursa ya kutumia Tehama ktk juhudi za kupambana na umasikini hapa nchini.

Popular Posts

Labels