Saturday, March 14, 2015
MTANZANIA ABUNI NA KUTENGENEZA PROGRAM TUMISHI YA KITABU CHA NYIMBO ZA KRISTO KATIKA VIFAA VYA APPLE
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Union Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania Gideon Msambwa ameweka historia ya kuwa mtanzania wa kwanza kubuni na kutengeneza program tumishi ya kiswahili ya kitabu cha nyimbo za Kristo zinazotumiwa na waumini wa kanisa hilo ambayo ni program pekee ya nyimbo za injili kwa lugha hiyo kubuniwa na kutumiwa katika vifaa vya mawasiliano vya kampuni ya Apple duniani.
Gideon Msambwa ameiambia blog hii kuwa program hiyo iliwezeshwa na Apple kupatikana katika vifaa vya mawasiliano vinavyoendeshwa na program ya endeshi ya iOS ambavyo ni iPhone,iPad na iPod na imeanza kutumika rasmi Machi 12,2015.