Saturday, January 21, 2012

WATEJA WA CRDB SASA KUWEKA NA KUTOA FEDHA KWA M-PESA

WATEJA wa Vodacom M-Mpesa wenye akaunti katika benki ya CRDB sasa wanauwezo wa kuweka na kutoa fedha kutoka katika akaunti zao kupitia simu ya mkononi ya Vodacom iliyosajiliwa na huduma ya M-Mpesa.

Kuzinduliwa kwa huduma hiyo sasa kunawapa urahisi zaidi wateja wa Vodacom M-Mpesa kuweka na kuchukua fedha zao kutoka akaunti ya benki kwa urahisi na unafuu zaidi mahali popote nchini na kwa wakati wowote pasi na kulazimika kufika katika tawi la benki ya CRDB..

Huduma hii ya ushirikiano kati ya Benki ya CRDB na kampuni ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-Mpesa ni ya kwanza nchini na inalenga kuwaondolea usumbufu wateja wa M-Mpesa wa kupanga foleni ama kutembea umbali mrefu kufuata tawi la Benki.

“Tunapoitambulisha huduma hii mpya inaamaanisha kwamba tumeongeza thamani nyengine katika simu ya mkononi na huduma ya Vodacom M-Mpesa. Mteja wa M-Mpesa kuweza kutoa na kuchukua fedha kutoka akaunti zao za CRDB kupitia simu zao za mkononi ni hatua nyengine muhimu ya kujivunia kuwa mteja wa Vodacom”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza.

Huduma ya Vodacom M-Mpesa ya kwanza sokoni kutoka Vodacom mtandando unaoongoza nchini ni kielelezo makini cha ubunifu na namna ambavyo Vodacom imedhamiria kubadili maisha ya watu kupitia teknolojia ya simu za mkononi.

Ikiwa na mawakala zaidi 20,000 nchi nzima M-Mpesa inabakia kuwa huduma salama zaidi, ya haraka, uhakika na yenye kuaminika kwa ajli ya kuweka na kutuma fedha, kufanya malipo ya huduma na manunuzi mbalimbali, kulipia kodi, kuchangia pensheni pamoja na kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya sabini na tano ulimwenguni.

“Hakuna mteja wa Vodacom M-Pesa atakaesimama kwenye foleni au kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata tawi la benki yake ya CRDB, sasa wataweka na kutoa fedha wakati wowte na mahali popote bila kuathiri shughuli nyengine za kijamii na kimaendeleo ni wazi maisha yamekuwa rahisi zaidi.”Aliongeza Bw. Rene

Tangu ilipoanzishwa mwaka 2007, huduma ya Vodacom M-Mpesa imeendelea kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuwa huduma yenye usalam zaidi, yenye mtandao mpana wa mawakala mijini na vijijini na hivyo kuchangia maendeleo ya jamii na biashara nchini kwa kuinua vipato vya wananachi kupitia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Kuweka fedha katika akaunti ya CRDB kutoka akaunti ya M-PESA,hatua ni kama ifuatavyo
I. Piga *150#
II. Chagua kulipia bili
III. Ingiza namabri ya biashara ambayo ni 900500
IV. Ingiza nambari ya kumbukumbu ambayo ni namabri ya akaunti ya benki.
V. Weka kiasi cha fedha mteja anachotaka kutoa katika akaunti ya M-PESA kwenda akaunti ya benki
VI. Ingiza nambari ya siri.
VII. Bonyeza 1 kuthibitisha au 2 kubatilisha muamala.
Baada ya hatua hizi mteja atapokea mara moja ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA kuthibitisha muamala na baada ya dakika 8 atapokea ujumbe kutoka benki ya CRDB.
Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya Benki ya CRDB kwenda M-PESA hatua ni kama ifuatavyo
I. Piga *150*03#
II. Ingzia nambari ya siri
III. Chagua nambari 3 (Hamisha fedha)
IV. Chagua nambari 3 (M-PESA)
V. Chagua nambari ya akaunti yako ya Benki
VI. Thibitisha nambari yako ya simu
VII. Ingiza kiasi cha fedha unachotaka kuhamisha
VIII. Thibitisha au batilisha. Na baada ya hapo utapokea ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA na pia Benki ya CRDB unaothibitisha zoezi hili.
Ili kuwa na uwezo wa kuhamisha fedha kutoka Benki kwenda M-PESA ni LAZIMA kwanza mteja wa M-PESA ajisajili CRDB.
Usajili huo hufanyika MARA MOJA TU na kwamba unaweza kufanyika kupitia simu ya mkononi kwa kupiga *150*03# na maelezo ya namna ya kujisajili yatatotekea ambayo mteja atapaswa kuyafuata.

WIZI WA TAARIFA KWA MTANDAO NA NJIA ZA KUKABILIANA NAO

Dunia ya ulinzi na usalama wa masuala ya mawasiliano inapitia kipindi kigumu kwa kipindi cha miaka 5 sasa ambapo wahalifu wengi wamekuwa na ushindani wa kuiba taarifa mbalimbali kwa njia ya mtandao ili kuweza kuzitumia taarifa hizo kwa ajili ya shuguli mbalimbali kutegemeana na uhitaji wa taarifa hizo .

Katika dunia ya uhalifu kwa njia ya mtandao haswa unaohusu taarifa
kuna makundi 5 yanayojulikana zaidi kutokana na nia zao za kuiba taarifa hizo .

Kundi la kwanza ni la wahalifu wa kifedha hawa wanaiba taarifa pale
ambapo unaingiza taarifa zako kwenye mitandao usiyoijua taarifa hizo zinahifadhiwa sehemu fulani kwa ajili ya kutumika sehemu nyingine za dunia hawa mara nyingi wanahamisha fedha kwa kutumia taarifa walizopewa na mtu asiyejua vyema kile anachokifanya kwa njia ya mtandao .

Kukabiliana nayo
Kuna benki zenye vifaa vinavyoitwa KeyChanger hiki ni kifaa unachokuwa nacho mkononi kama flashdisk au remote control pindi unapotaka kuingia kwenye akaunti yako ya benki kwa njia ya mtandao unabonyeza kifaa hicho na kupatiwa Password Mpya .

Sio benki zote zenye huduma hizi na mara nyingi inategemea na kiasi

cha hela ulichonacho kwenye benki husika yaani mteja wa aina gani .

Geo Location

Geo Location ni tabia za mtumiaji wa huduma za kibenki pale alipo ,benki nyingi hazina utaratibu za kujua tabia za mteja wao na
kumfuatilia pale anapochukulia hela mara kwa mara au tarakilishi
anayotumia kuingilia kwenye mtandao wa benki hiyo mara kwa mara

Benki zikianzisha Geo Location kwenye uchukuaji wa pesa ina maana kama
mtu yuko Dar es salaam na amekuwa anachukulia pesa Dar es salaam tawi la Mlimani City kwa mfano akihamia Mwanza asiweze kutoa fedha kwa muda huo mpaka aweze kudhibitisha taarifa zake au mtu akiwa Kenya na kufungua akaunti hiyo hiyo asiweze kufanya hivyo bila kujibu baadhi ya maswali kwa mfano mara ya mwisho kutoa hela alitumia tawi gani tarehe ngapi .

Kundi la pili na ambalo linakuja juu zaidi ni uhalifu au uharamia wa
mtandao kwa ajili ya kutafuta taarifa kuhusu Taifa fulani , vikundi fulani vya watu wanaotumia mitandao kuwasiliana zaidi mitandao jamii na wavuti za serikali za nchi wanazopingana nazo au za wanaharakati au vyama vya siasa labda upinzani au vinavyotawala .

Kukabiliana nayo

Kwa serikali na taasisi nyingine nyeti ni vizuri kuwa na programu na mifumo imara ya mawasiliano na kuwa na watu wa ulinzi na usalama kwa njia ya mtandao , pili ni kwa serikali na taasisi zake kufanya mabadiliko kwenye programu( customise ) wanazotumia katika tarakilishi zao ili ziweze kuendana na mazingira yao pamoja na mahitaji yao .

Nchi zilizofanikiwa zaidi kwa kubadilisha programu ni Umoja wa Ulaya
ambao umeingia mkataba maalumu na kampuni zinazotengeneza programu hizo kama Microsoft , oracle ,Adobe ,Symantec

Kundi la tatu ni wale wanaoiba taarifa kwa nia tu ya kutangaza bidhaa
zao au huduma zao nyingine kutumia anuani pepe haswa zile za bure kama yahoo ,hotmail hii imeathiri watu wengi wa nchi maskini haswa chini ya jangwa la sahara ambapo hawana uwezo mkubwa wa kukabiliana na baadhi ya vitu vipya kwenye teknologia .

Kukabiliana nayo

Kitu cha muhimu ni kwa watu kuacha kutumia barua pepe za bure sasa hivi kusajili rajisi Domain ni bei ndogo sana unaweza kusajili domain name yako kama www.mwanahawa.co.tz kwa ajili ya wakazi wa tanzania au www.mwanahawa.co.ke kwa wakazi wa kenya chochote kikitokea hapo unaweza kupata kwa urahisi kutoka kwa msajili wa rajisi hizo kwa tanzania ni www.tznic.or.tz

Kundi la nne ambalo sipendi kuliongelea sana ni wale wanaoiba na

kuzichapisha kwa nia ya kuharibu taswira ya mtu , mataifa , makundi mengine ya jamii haswa wale wanaopingana nao au wanaoona hawafanyi kazi vizuri na kuwajibika hawa wengi wako kwenye mitandao jamii kama wikileaks na zambiawatchdog .

Kukabiliana nayo

Hii ni ngumu kidogo maana inategemea taarifa zimetokea wapi kama ni Hardcopy au Softcopy kukabiliana na hali hii ni kutumia mifumo
endelevu ya digitali kwa ajili ya kuhifadhi taarifa kama ni kwa njia ya karatasi au kwa njia Mtandao na wafanyakazi wa sehemu nyeti kuchukuliwa alama zao za vidole na nyingine ili ziweze kutumika endapo taarifa zimevuja au kwenda kwenye mikono ambayo sio sahihi

Kundi la 5 ni mafundi au watumiaji wengine wa tarakilishi ambao

wanaweza kuiba taarifa zako kwa njia ya vihifadhi kama
flashdisk ,Cd ,au kama kuna mtandao wanaweza kuzirushia kwenye mtandao hapo hapo zaidi kuhusu mafundi wa tarakilishi ni pale unapopeleka kompyuta yako kwake kwa ajili ya matengenezo hapo taarifa zako zinaweza kuibiwa .

Kukabiliana nayo

Hakikisha Taarifa zako nyeti unaondoa kabla ya kupeleka kifaa chako sehemu za mbali kwa ajili ya matengenezo ingawa mtu ataweza kupata taarifa hizo kwa kutumia program nyingine za kurudisha taarifa hizo ( recovery ) njia bora zaidi ni kuwa na watu wako wa kurekebisha matatizo ya ufundi ambao una mikataba nao inayohusu uhifadhi wa taarifa ( data act )

Taarifa nyingi sana zimekuwa zikiibiwa na kutumika ndivyo sivyo na
vyombo vingine lakini pia vyombo vingine havijachoka kubuni na
kutengeneza program mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa mali za watu , suala lililo kuu kuliko yote ni kwa mtu mwenyewe , taasisi au serikali kuwafunzi wafanyakazi wake kuhusu taratibu nzuri za kuhifadhi taarifa na kuzitumia haswa kwa njia ya mtandao , kuwa na program nzuri za ulinzi na usalama ambazo ziko updated na wenyewe kupenda kutafuta taarifa na maarifa zaidi kuhusu ulinzi na usalama wa mali zao kwa njia ya mtandao .

Njia nyingi hapo kuweza kuzitumia sawa sawa ni gharama na zinahitaji
uwekezaji haswa kwa muda mrefu kwa njia ya elimu ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhalifu huu .

YONA FARES MARO

DAR ES SALAAM
+255786806028

Friday, January 20, 2012

MAHUSIANO KUPITIA FACEBOOK YASABABISHA MAUAJI

Abuja, Nigeria
UHUSIANO wa kimapenzi, ulioanzishwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, umesababisha kifo cha mrembo nchini Nigeria.
Habari za mtandaoni zinadai kuwa mrembo huyo (jina halikutajwa) pamoja na boyfriend wake (jina pia halijatajwa), walikuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu.

Imedaiwa kuwa wakati wawili hao wakiwa kwenye utekelezaji wa hatua za mwanzo za kufunga ndoa, mrembo huyo alimtaarifu boyfriend wake kuwa amepata mpenzi mwingine kwa njia ya Facebook.
Chanzo cha habari kiliiambia tovuti moja ya nchi hiyo kwamba mrembo huyo alianzisha urafiki wa Facebook na kijana mmoja raia wa Marekani (jina halijatajwa) kabla ya kibao kubadilika na kuwa wapenzi.

Chanzo kiliendelea kupasha habari kwamba mrembo huyo na mpenzi wake wa Facebook, walidumisha uhusiano wao kwa njia ya mawasiliano ya simu kwa muda mrefu kabla ya kukata shauri la kuonana ana kwa ana.

“Yule kijana raia wa Marekani alitembelea Nigeria, akafikia hoteli moja kubwa. Yule mrembo akaenda kukutana naye na kutumia muda mrefu chumbani.

“Ni kama baada ya kukutana ndiyo mapenzi yaliongezeka zaidi, kwani alipoondoka hotelini, yule mrembo alirudi kwa boyfriend wake aliyepanga kufunga naye ndoa na kumueleza kwamba mapenzi yamekwisha.

“Baada ya kuambiwa hivyo, kijana aliyekuwa na mategemeo ya kufunga ndoa na mrembo huyo, alimpeleleza mpenzi wake na kubaini mahali ambako kijana kutoka Marekani alifikia.
“Siku iliyofuata alivamia kwenye ile hoteli, akamkuta mpenzi wake na yule kijana wa Facebook, hapo ugomvi mkubwa ulizuka. Ugomvi haukuishia hapo kwa sababu kijana wa Nigeria aliahidi ni lazima aue mtu.

“Siku moja baada ya ugomvi hotelini, kijana wa Nigeria alimteka mpenzi wake na kumuua kwa kumkatakata na silaha inayodhaniwa kuwa ni panga,” alisema mtoa habari huyo.
Kwa mujibu wa mtandao huo mpaka pale habari hiyo inachapishwa, mtuhumiwa wa mauaji alikuwa hajakamatwa.

Saturday, January 7, 2012

MUELEKEO MPYA WA SEARCH ENGINES

Miaka 10 iliyopita watu wengi walitumia search engines kwa ajili ya kutafuta vitu kwa njia ya mtandao zaidi ilikuwa ni viunganishi vya vitabu habari mbalimbali kuhusu watu au mambo wanayoyataka wao na wavuti nyingi za search engines zilikuwa na njia hiyo moja tu haikumpa mtu fursa zaidi kama akitaka ilibidi mpaka aingie kwenye wavuti husika .

Miaka 5 iliyopita  kampuni za search engines duniani zilibadilika kwa
kiasi kikubwa mpaka sasa hivi ambapo mtu unaweza kutafuta jambo Fulani na ukaamua kama unataka kuona picha yake tu au unataka nyaraka yake kwa mfumo wa pdf tu au mawasiliano tu na fursa nyingine nyingi kutumia mtandao .

Katika kipindi hicho cha miaka 5 iliyopita taasisi za elimu

ulimwenguni na kampuni mbalimbali ziliingia zaidi kwenye utafiti wa kufanya search engines ziweze kutafuta vitu maalumu kwamba sasa kuwe na search engines za vitu maalumu kama ni daktari aweze kutembelea search engine yenye vitu anavyotaka yeye na sio majibu anayotaka yahusiane na vile asivyotaka yeye .

Sasa hivi kuna search engine za vifaa vya magari tu kwa njia ya
mtandao , kuna pia za vioo tu aina mbalimbali za vioo , kuna search engine za kutafuta nyaraka za PDF tu au Nyaraka za Doc za Microsoft word tu na nyingine nyingi sana .

Pia wengine walifanya utafiti kuona wanavyoweza kutumia search engines
na program nyingine za tarakilishi kuweza kutafuta vitu na kuvitambua katika muda mchache nap engine kupata taarifa zaidi kuhusu kitu hicho .

Mimi ni mmoja ya watu walioingia kwenye utafiti huu kwa kipindi hicho
kwa kushirikiana na chuo kimoja pamoja na mashirika kadhaa ambapo kwa kiwango kikubwa sana nimeweza kupata majibu na kuweza kuendeleza mengi zaidi

SABABU KUU

Kilichonifanya kuingia kwenye shuguli hii ni Filamu ya Black Hawk Down
iliyokuwa inahusu shuguli za wajeshi wa marekani nchini Somalia .

Kuna tukio moja ambapo Helcopter ya Jeshi ilikuwa inataka kufanya

shambulio mahala lakini hawakujua haswa ni nani aliyekuwepo kwenye jengo hilo na wanajeshi waliokuwa ardhini hawakuweza kuonekana kilichokuwa alama yao kuu ni Gari yao wenyewe iliyokuwa ina alama juu ambayo ndio rubani wa helcoper aliangalia .

Hii filamu ni ya zamani kidogo lakini mpaka siku za karibuni majeshi
na vyombo vingi vya usalama vimeshindwa kupata taarifa sahihi za mtu au kitu wanachotafuta matokeo yake ni kuumiza wengi zaidi na kuharibu mali .

Hata kwenye uvamizi wa jeshi la kesho nchini Somalia sasa hivi

kumeonyesha udhaifu huo huo wa kutopata taarifa sahihi kabisa kabla ya kufanya shambulio .

KILICHOFUATIA .

Kwa sababu nimekuwa kwenye Uendelezaji wa Programu za Google Earth na hii ndio ilikuwa nyenzo yangu muhimu kwa kushirikiana na Huduma nyingine za Kampuni la Google na Search engine tofauti na Mitandao mengine ya Jamii .

Google Earth bado ina huduma nyingine nyingi za kufanyia utafiti zaidi
na kazi ili kuweza kupata bidhaa mbalimbali kama hii yangu

MATOKEO YAKE .

Kwa sasa hivi Tunaweza kupata halaiki ya watu zaidi ya alfu 6
waliokusanyika sehemu moja na kuweza kutambua sura za watu hao kisha kupata taarifa zao nyingine zilizohifadhiwa kwenye database katika kipindi kifupi sana kama mtu huyo alikuwa anatafuta kwa njia yoyote ile ni rahisi kupatikana kama alikuwa kwenye halaiki hiyo .

Kama kuna hatari zozote za mafuriko , moto na majanga mengine mfumo
huu unaweza kutoa taarifa za kina kwa wadau mbalimbali na wataweza kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti hali au hata kuwasiliana na wale waliochini.

HII NI KIFUPI KUHUSU MUELEKEO WA SEARCH ENGINES
Karibuni kwa maoni mbalimbali na maswali mbalimbali .
Sijaandika kitaalamu zaidi kuhusu kitu hichi ili watu waweze kuuliza
maswali na nijibu lakini msiogope .
Yona Maro-+255786 806028 au oldmoshi@gmail.com

Popular Posts

Labels