Wednesday, December 31, 2014

TUUFUNGE MWAKA NA KUANZA MWAKA KWA KUJIHADHARI NA UHALIFU MTANDAO

 
Mwaka 2014 Umekua wenye changamoto nyingi sana kwenye upande wa mitandao ambapo wahalifu mtandao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuitikisa anga ya usalama mitandao duniani kote ambapo walifikia kutamba kuwa wameshinda mapambano na wanausalama mitandao.

Kubwa zaidi ni uelewa mdogo wa watumiaji mtandao juu ya kujiweka salama kimtandao iliyoambatana na wana usalama mitandao kuwa wachache sana katika ngazi ya kidunia huku baadhi ya mataifa kutotoa kipaumbele katika maswala ya usalama mitandao.

Aidha, Mengi katika jitihada yameweza kufikiwa ikiwa ni pamoja na Kikao cha funga mwaka cha tathmini ya hali ilivyokuwa kwa mwaka 2014 ambapo iliweza kutabiri hali ya uhalifu mwaka 2015 na kuweka mikakati ya dhati ya kukabiliana na hali hiyo kwa mwaka 2015 inayotegemewa kuwa na matokeo chanya. Kwenye hili unaweza kulisoma kwenye  “TAARIFA FUPI INAYOSOMEKA HAPA"

Wamarekani nao kupitia “US department of Justice” wameamua kuazisha kitengo maalum kitakachotoa msaada kwa mataifa yote duniani katika upande wa maswala ya usalama mitandao ikisisitiza itaangazia zaidi katika kuzuia matatizo kabla hayajatokea.

Tanzania nayo haikubaki nyumba kwenye hili, Tumeshuhudia warsha, semina, kongamano na mikutano mingine yenye malengo thabiti ya kukuza na kuongezea uwezo wa uelewa wa matumizi salama ya mitandao paoja kukuza uwezo wa kukabiliana na hali ya uhalifu mtandao nchini.


Sheria za usalama mitandao zimeweza kupaziwa sauti na kutoa matumaini makubwa kwa mwaka ujao, Huku vyombo vya habari kuw na jitihada ya dhati katika kampeni ya kutoa elimu na kuhabarisha jamii kuhusiana na janga la uhalifu mtandao linaloweza kuleta athari zaidi kwa taifa.

Nikumbushe tu, Uhalifu Mtandao umeendelea kuja kwa kasi ya juu na njia ambazo watanzania wengi wameweza kuwa waathirika. Kubwa nililoliona ambalo kueleke mwisho wa mwaka limeweza kukamata kasi ni pamoja na uhalifu aina ya “Phishing kama unavyo onekana kwenye picha nilizo tumiwa na baadhi ya raia wema ambapo wengi wameendelea kuathiriwa na uhalifu huu wa kimtandao.
Umakini zaidi unahitajika na tumalize mwaka kwa kuwa salama kimtandao.
Na:Yusuph Kileo

Wednesday, December 24, 2014

SEMINA YA USALAMA KATIKA MITANDAO YAFANYIKA DIT



Mtaalaam wa Masuala ya Usalama kwenye Mitandao Yusuph Kileo akitoa mada





Mshiriki akiuliza swali

Mshiriki wa Semina akiwa ameshikilia zawadi yake baada ya kujibu maswali

Washiriki wakiuliza maswali

Desemba 23 mwaka huu mtalaamu wa masuala ya usalama kwenye mitandao Yusuph Kileo aliendesha semina ya usalama mtandaoni iliyofanyika Dar es salaam Institute of Technology (DIT) na kuhudhuriwa na wanafunzi mbalimbali wa teknolojia ya habari na mawasiliano toka miongoni mwa vyuo vikuu vya jijini Dar es salaam,ikiratibiwa na DIT.

Katika semina hiyo Kileo alielezea ukuaji wa uhalifu kwenye mtandao unavyoendelea kushamili kwa kasi duniani na unavyoleta athali mbalimbali za kiuchumi,kiusalama na kisiasa huku nchi mbalimbali zikiathilika ikiwemo Tanzania huku ikionekana kuwa nchi zinazoendelea bado hajijajidhatiti barabara katika kujilinda na wahalifu wa kwenye mitandao.

Kileo amewataka wanafunzi waliohudhuria semina hiyo kujifunza zaidi masuala ya usalama kwenye mitandao kwani kuna watalaam wachache katika suala  hilo na amesema kuna haja ya vyuo vinavyotoa elimu ya teknohama nchini kuweka somo la usalama kwenye mtandao katika mitaala yao ambapo amesema wamekubaliana na DIT kuipitia mitaala ya taasis hiyo ili mapema mwakani somo hilo lianze kufundishwa kwenye taasis hiyo.

Friday, December 19, 2014

KASISI AWEKA KIFAA KANISANI KUBANA MAWASILIANO YA SIMU KWA WAUMINI



 

Kasisi mmoja nchini Italia, ameweka kifaa kanisani mwake kinachoweza kubana mawasiliano ya simu baada ya kuchoka kuwaomba waumini kuzima simu zao kila wakati alipokuwa anahubiri.

Alilazimika kuomba idhini ya polisi kuweka kifaa hicho baada ya kuchoka kusikia milio ya simu zikipokea ujumbe.

Mpango huo umesifiwa sana na waumini ingawa imewaudhi wenye maduka katika mji wa Naples wanaosema kifaa hicho kinatatiza masafa na mawasiliano yao na pia kifaa hicho kimeathiri mashine za kutoa pesa.

Wanasema kifaa hicho pia kinatatiza shughuli zao ambapo wateja huagiza bidhaa kupitia simu zao za mkononi.

Kasisi Don alikasirishwa sana na waumini wake kujibu simu zao wakiwa kanisani

Lakini kasisi Don Michele Madonna, anakana kwamba kifaa chake kinatatiza shughuli za wenye maduka akisema kinaathiri tu mawasiliano kwa simu kwa waumini walio kanisani peke yake.

'Nilinunua kifaa hicho kutoka kwa duka la vifaa vya elektroniki, na kuwauliza polisi ikiwa ilikuwa sawa kuweka kifaa hiicho kanisani mwangu. Ni kifaa kizuri sana kwa sababu kimemaliza tatizo la watu kupigiwa simu na kuzipokea wakiwa kanisani.

Mmiliki mmoja wa maduka alisema: 'Tangu kasisi Madonna kuweka kifaa hicho ndani ya kanisa , nimepata matatizo sana kutumia kadi yangu katika biashara yangu. ''


Kasisi Michele Madonna aliamua kuchukua msimamo huo kwa sababu waumini walikuwa na mazoea ya kutumia simu zao kanisani wakati kasisi huyo akihubiri. Kilichomuudhi zaidi kasisi huyo ni watu kupokea simu kanisani na hata wakati wa mazishi.

Kasisi Don alinunua kifaa hicho kwa dola sitini.

Kabla ya kukinunua kifaa hicho alianza kwa kuwasihi waumini kutotumia simu zao kanisani kwa sababu zilitatiza shughuli zake.

 Alianza kwa kuweka mabango kanisani humo lakini ujumbe huo wengi hawakuuzingatia na hapo ndipo akalazimika kuweka kifaa hicho ambacho kinazuia watu kupokea au hata kutumia simu zao kanisani.

Saturday, December 13, 2014

MANISPAA YA KINONDONI YAZINDUA HUDUMA YA BURE YA INTANETI KWENYE KITUO KIPYA CHA DALADALA CHA SINZA

 
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akibofya kompyuta kuzindua huduma ya WiFi ya bure kwenye Kituo cha Mabasi cha Sinza, wilayani humo, Ijumaa, Desemba 12, 2014
Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imedhihirisha jitihada zake za kwenda na wakati katika masuala ya teknohama, baada ya kuamua kutoa huduma ya bure ya mtandao wa intaneti wa WiFi kwenye Kituo kipya cha Mabasi cha Sinza, jijini Dar es Salaam.
Akizindua huduma hiyo Desemba 12, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda amesema, mtandao wa WiFi umeunganishwa kwenye kituo hicho kupitia mkongo wa mawasiliano kupitia Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Mwenda amesema, mtandao huo utakuwepo usiku na mchana na kila mwenye kompyuta au simu zenye uwezo wa kunasa Wi-Fi ataona katika simu au kompyuta yake akitaarifiwa kuwepo mtandao wa bure wa KMC_FREE WiFi.
Alisema, mdau atakachofanya ni kujinga bure na kuendelea kupata taarifa mbalimbali zikiwemo za tovuti ya serikali na ya Manispaa hiyo ya Kinondoni na nyingine zote atakazotaka.

Mwenda amesema, baada ya kuweka mtandao kwenye Kituo hicho, mwakani Manispaa hiyo itaweka mtandao huo wa WiFi kwenye Kata zote 34 za Manispaa hiyo.
Amesema, mradi huo wa WiFi umegharimu sh. milioni 21, na Manispaa hiyo itakuwa ikiendelea kulipia huduma hiyo sh. milioni 2 kila mwezi ambazo itakuwa inalipa kwa mkupuo kwa mwaka. Kuzinduliwa kwa huduma hiyo, kumeifanya Manispaa ya Kinondoni kuwa ya kwanza nchini kote, na pengine hata Afrika Mashiriki, kutoa huduma hiyo bure tena bila kutumia namba ya siri.
Huduma inayofanana na hii hupatikana katika nchi mbalimbali zilizoendelea dunian.
Chanzo:Bongonewstz.com 

Thursday, December 4, 2014

RAIA 77 WA UCHINA WASHTAKIWA KENYA KWA TUHUMA ZA UDUKUZI NA ULANGUZI WA FEDHA



 

Polisi nchini Kenya wamewafikisha mahakamani raia 77 wa Uchina kwa kushukiwa kushiriki udukuzi wa mawasiliano na ulanguzi wa fedha.
Washukiwa hao wamewekwa rumande kwa siku tano zaidi ili kutoa nafasi kwa polisi kufanya uchunguzi wa kina.

Wakili wa washukiwa hao anataka waachiliwe kwa dhamana na ombi lake litasikizwa kesho katika mahakama kuu mjii Nairobi.

Washukiwa hao 77 walikamatwa katika nyumba moja kwenye mtaa wa kifahari wa Runda jijini Nairobi Jumatatu na jumatano wiki hii na wanadaiwa kushiriki katika vitendo vya udukuzi na ulanguzi wa fedha.
Upande wa mashtaka uliomba mahakama muda zaidi kuwachunguza washukiwa hao.

Hata hivyo wakili wa washukiwa hao Tom Wachakana aliishawishi mahakama kusikiza ombi lake kutaka washukiwa waachiliwe kwa dhamana.
Wakati maafisa wa polisi walipovamiwa makazi ya washukiwa hao walipata mitambo ya teknolojia ya hali ya juu inayodhaniwa inatumika kufanya ujanja katika mitandao.

Mbali na maafisa wa polisi, wakuu katika wizara za mambo ya nje na habari na mawasiliano walihusishwa katika msakao huo. Afisa katika ubalozi wa Uchina mjini Nairobi ambaye hakutaka kutajwa aliiambia BBC kuwawatashirikiana na serikali ya Kenya inayochunguza asili ya raia hao katika kuangalia stakabadhi zao za usafiri.

Washukiwa hao wamekamwatwa wakati kampuni nyingi za Kichina zimewekeza katika biashara hasa katika sekta ya ujenzi.

Kadhalika serikali ya Kenya imetia saini mikataba mingi na wachina huku baadhi yao wakihusisha katika miradi ya serikali hususan katika taasisi za elimu ya juu.
Chanzo:BBC

Popular Posts

Labels