Thursday, December 15, 2016

YAHOO YASEMA WATUMIAJI BILIONI 1 WA MTANDAO HUO WAMEATHIRIWA NA WAVAMIZI WA MITANDAO



 Kampuni ya Intaneti ya Yahoo inasema wavamizi wa mitandao waliiba data za zaidi ya ya watumiaji wake bilioni moja. Tukio hilo linaaminika kufanyika mnano mwaka 2013. 
Katika taarifa yake, Yahoo inasema uvamizi huo wa taarifa muhimu ni tofauti na ule ulioripotiwa mwezi Septemba mwaka huu, ambapo wavamizi hao waliiba taarifa kutoka kwenye akaunti mbalimbali za watumiaji zaidi ya milioni mia tano.



Imeongeza kuwa data zilizoibiwa zinajumuisha majina, anuani, namba za simu,tarehe za kuzaliwa pamoja na nywila (namba za siri).

Lakini kadi za malipo sambamba na akaunti za benki hazikuingiliwa.

Wednesday, December 14, 2016

KAGOYA YASHAMBULIWA KIMTANDAO – TANZANIA NAYO YAASWA KUFUNGA MIKANDA

Kampuni Maarufu ya KAGOYA ya Nchini Japan Imeshambuliwa kimtandao ambapo taarifa binafsi na za kibenki za wateja wake zimedukuliwa.

Uhalifu huu umegundulika mwezi huu (Desemba, 2016) na tayari kampuni husika imesha toa taarifa kwenye vyombo vya usalama vya Nchini humo - Ambavyo pia vimeanza uchunguzi rasmi.

Kampuni hiyo imesema, Wateja wake waliotumia "Credit card " zao baina ya Aprili Mosi , 2015 hadi september 21, 2016 wameathiriwa na uhalifu huu na imewaasa wateja wake wafatilie taarifa za utoaji pesa wa kadi zao.

Taarifa binafsi takriban Elfu 50 pamoja na taarifa za kibenki takriban Elfu 21 zimeathirika katika shambulio hili la kimtandao.

Mjumuiko wa taarifa zilizo ibiwa ni, majina , barua pepe, Namba za simu, Namba za kadi za benki, maneno ya siri (Nywila) pamoja na taarifa nyingine za wateja wake.

Hii si mara ya kwanza kwa Nchi ya JAPANI kupata shambulio kubwa la kimtandao kwa mwaka huu (2016) pekee - Itakumbukwa, Mwezi May mwaka huu (2016) zaidi ya Yuan Bil. 1.5 sawa na Dola Milioni 13 ziliibiwa katika ATM zaidi ya 1400 ndani ya masaa mawili na nusu.



Aidha, TANZANIA hali ya uhalifu mtandao bado ni changamoto inayo hitaji suluhu ya kudumu. Kuibiwa kwa Fedha na Taarifa , Matumizi mabaya ya mitandao, Tovuti kudukuliwa ni miongoni mwa matukio yaliyo jitokeza kwa mwaka huu 2016.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (UUW) imeleza Waziri mwenye dhamana wa wizara hiyo ametaka kupatikana kwa mwarobaini wa wimbi la wizi mtandao unapatikana Nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi Bodi ya TCRA (Mamlaka ya Mawasiliani Tanzania)  Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya TCRA, kuhakikisha wanapata mwarobaini wa kudhibiti ongezeko la wizi wa mitandao unaoendelea kukithiri hapa nchini.

Prof. Mbarawa amesema watanzania wameibiwa kwa muda mrefu kupitia njia ya ujumbe mfupi na kushawishiwa kutoa fedha kwa njia ya udanganyifu na hivyo kuitaka bodi hiyo kutofumbia macho changamoto hiyo.

“Changamoto ya wizi wa mitandao inagusa watanzania wengi, mkiwa na jukumu la kudhibiti mna wajibu wa kuwalinda wananchi”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa bodi hiyo ihakikishe inasimamia kwa karibu sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa katika kudhibiti ubora wa masuala ya mawasiliano ikiwa ni teknolojia inayokuwa kwa kasi kubwa.

Aidha Prof. Mbarawa ameitaka bodi hiyo kuendelea kudhibiti wimbi la meseji za uchozezi zinazotumwa na baadhi ya wananchi kwa kukosa maadili.

Katika kuimarisha huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Waziri Prof. Mbarawa ameikata TCRA kufanya maamuzi ya haraka na kuwa wabunifu ili kuweka mazingira endelevu ya kukuza sekta hiyo.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TCRA Dkt. Jones Kilimbe amesema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo, Bodi itahakikisha inapata suluhu ya changamoto hizo ndani ya muda mfupi.
Hatuna Budi kutambua kua janga la uhalifu mtandao ni kubwa na athari zake zimekua zikionekana situ kwa nchi zisizo na teknolojia nzuri ya kukabiliana na uhalifu mtao bali pia Nchi zilizo endelea zimekua wahanga wa janga hili.

Taifa la Tanzania halina budi bali kuanza na utayari uliombatana na kujipanga upya na vizuri kukabiliana na Wimbi la uhalifu mtandao nchini.

Changamoto za urasimu, matumizi makubwa ya pesa kwenye kampeni za kukuza uelewa zinazokosa matokeo chanya pamoja na kutojiongezea elimu ya mara kwa mara ya kukabiliana na uhalifu huu mtandao lazima ipaiwe suluhu.

Sheria Mtandao pekee haziwezi kutuvusha kwenye wimbi hili la ukuaji wa uhalifu mtandao nchini, Lazima mambo mengine muhimu ya kukabiliana na uhalifu mtandao yafanyiwe kazi.

Naziasa taasisi binasfi na za serikali kujenga tabia ya kutoa taarifa ya matukio ya kishambulizi mtandao mara tu yanapo gundulika ili iwe rahisi kupatiwa suluhu. Bila kufanya hivyo wahalifu mtandao wataendelea kupata nguvu.

Kwa sasa Tanzania, Hatujafikia pabaya sana kulinganisha na mataifa mengine – Ila, Kama hatua za haraka na za dhati za kujipanga na kufunga mikanda hazitachukuliwa mapema, Mbele yetu ni mbaya Mno.

Kumeonekana mapungufu makubwa maeneo mbali mbali Nchini ambayo yanaweza kupelekea taifa kutumbukia kwenye hali mbaya ya uhalifu mtandao ambapo taarifa na tafiti mbali mbali zinazo fanywa nchini na nje ya nchi zime baini mapungufu mabali mbali yanayoweza kupelekea wadukuzi kutuingiza matatizoni.
Na:Yusuph Kileo


Tuesday, December 6, 2016

TUZO ZA UMAHILI KWA WAANDISHI WA BLOG ZAJA


Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wamiliki wa blog nchini humo inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.

Katika hotuba yake ya kufunga Mkutano Mkuu na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini jijini Dar es salaam leo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (Pichani)amesema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.

Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo na   makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.
Waziri Nape pia amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.

Monday, December 5, 2016

SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII (BLOG)

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.
Mwanahabari na Blogger  Frederick Katulanda (kulia), akiuliza swali.
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (kushoto), akiwaelekeza jambo mablogger


Mkutano ukiendelea.

Mablogger kazini

Blogger Baraka kutoka Bukoba akiuliza swali.
Mwezeshaji wa mkutano huo Maxsence  Mello akitoa mada.

Bloggers wakifuatilia mada.
Mwendeshaji wa mtandao wa FullShangwe, John Bukuku akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NMB wakibadilishana mawazo. Kushoto ni Doris na Joyce Nsekela.
Blogger kutoka mkoani Arusha, Tumaniel Seria (kulia), akiuliza swali. Kusho ni William Malecela mmiliki wa mtandao wa Mwananchi na katikati ni mmiliki wa Blog ya Michuzi Issa Michuzi.



Mmiliki wa mtandao wa Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda akichangia jambo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Serikali  imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Bloggers) kuwa chombo cha habari nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk.Hassan Abbas Dar es Salaam leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN).

"Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali" alisema Abbas.

Abbas alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.

Katika hatua nyingine Abbas alisema Bloggers haina tofauti na vyombo vingine hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weredi wa kazi vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo vingine. 

Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.

Wanamitandao hao  wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo kuwa  wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja na kunyimwa 'Press Card' jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.
Picha na Habari:Dotto Mwaibale


Sunday, December 4, 2016

YUSUPH KILEO MTANZANIA ALIYETWAA TUZO YA MWAKA YA USALAMA MTANDAONI


Yusuph Kileo baada ya kukabidhiwa tuzo


Mtaalamu wa masuala ya usalama mtandaoni Yusuph Kileo hivi karibuni alipata Tunzo ya "Cybersecurity expert of the year" Ikiwa ni katika kutambua mchango wake  katika mataifa ya Afrika.
 
Tuzo hizo zilitolewa Nairobi nchini Kenya ambapo Mgeni rasmi alikua ni PS au KM wa wizara ya mipango na Majimbo (Ugatuzi) - Kenya Mheshimiwa Saitoti Torome.Kwa ujumla zilitolewa tunzo 31 katika makundi tofauti.


CHAMA CHA WAMILIKI NA WAENDESHA MITANDAO YA KIJAMII KUFANYA MKUTANO WAKE MKUU

-->  
Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Wamiliki wa Blog (TBN),Joachim Mushi akizungumza na waandishi wa habari
Ofisa Uhusiano wa NMB,Doris Kilale akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 10 kwa Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Wamiliki wa Blog (TBN),Joachim Mushi kwa ajili ya mkutano mkuu utakaofanyika Desemba 5 hadi 6 jijini Dar es salaam


 Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' (TBN) kitafanya mkutano wake kwa siku mbili kuanzia kesho jijini Dar es salaam ukiwahusisha wanachana wake toka mikoa mbalimbali nchini.

Akitoa taarifa ya mkutano huo iliyoambatana na upokeaji wa hundi ya shilingi milioni 10 toka NMB Mwenyekiti wa muda wa TBN Joachim Mushi amesema lengo la mkutano huo ni wanatasnia kupewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kama ajira nyingine.
-->

Popular Posts

Labels