Saturday, August 17, 2013

TWITTER YAONESHA KUWAVUTIA VIJANA

 


Facebook ni mtandao wa kijamii ambao unaendelea kuongoza kwa kuwa na watumiaji wengi duniani hata hiyo utafiti unaonesha kuwa vijana sasa wanahama kutoka mtandao huo na kujiunga na mtandao wa kijamii wa Twitter .

Kuna mamia ya watu ambao haiwezi kupita siku bila kutembelea facebook,lakini sasa inaonekana twitter ikipata watumiaji kutoka facebook hasa ikiwavutia zaidi vijana ambao wengi wao wanatumia facebook.

Twitter inaruhusu mtumiaji kufahamu kile ambacho hadhira katika mtandao huo inakizunguzia na kuruhusu kufahamu kinachoendelea na kumpatia anachokihitaji.

Mtandao wa solidtechreview umeeleza kuwa mwishoni mwa mwaka  2012, inakadiliwa kuwa asilimia  21 ya watumiaji wa intaneti duniani walikuwa walikuwa wamejiunga na twitter na kila mwezi kulikuwa na watu milioni  288 waliokuwa wanajiunga na mtandao huo.

Utafiti unaonesha kuwa facebook ina asilimia 34 ya watumiaji ambao umri wao ni chini ya miaka  30 na asilimia 45 zaidi ya miaka  45. Wakati ni asilimia 30 tu ya watumiaji wa twitter ambao wanaumri zaidi ya miaka  45.

Twitter inaelezwa kuwa ni rahisi kutumiwa na watu ambao hawana muda mwingi wa kukaa na kuandika mambo mengi kwenye mitandao ya kijamii,rahisi kukuunganisha na watu wengi maarufu duniani, rahisi kuwasilianana kubadilishana mawazo mbalimbali kuliko facebook.

Popular Posts

Labels