Tuesday, August 27, 2013
TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA KOMPYUTA ZENYE WINDOW XP
Watumiaji wa programu ya komputa iitwayo Window XP wamepewa tahadhari na kampuni ya Microsoft ambayo ndiyo iliyotengeneza program hiyo kuwa hapatakuwa na matoleo mapya (updates) zaidi kuhusu Window XP Service Pack 3 baada ya mwezi wa nane mwaka 2014.
Akizungumza na wataalamu mbalimbali wa masuala ya ulinzi mtandao Agosti 16,mwaka huu Mkurugenzi wa kitengo kijulikanacho kwa jina la Microsoft Trustworthy Computing,Tim Rains anasema kuwa ingawa Window XP wakati inatolewa ilikuwa na ubora huku ikipendwa na watumiaji wengi wa kompyuta,kwa sasa imeonekana kuwa dhaifu kutokana na kuongezeka kwa uhalifu wa kimtandao.
Amesema kumekuwepo na wimbi kubwa la wahalifu wanaotumia mianya mbalimbali kuingilia kompyuta za wateja wanaotumia Window XP na kuongeza kuwa hali hiyo ya uhalifu itaendelea hasa kwa wale wataoendelea kutumia aina hiyo ya window.
Rains amesema wanaendelea kutafuta ufumbuzi pale itakapobainika wahalifu wameweza kupenya katika kompyuta za wateja wao wanaotumia aina mpya za window ambapo kwa sasa kupitia kituo cha kuangalia usalama wa kompyuta cha kampuni hiyo kinaendelea kutoa maelezo ya jinsi ya kuwalinda wateja wao.
Amesema kampuni ambazo bado zitakuwa zinatumia Window XP,zitasababisha wahalifu kutafuta mapungufu katika window hiyo na kuleta athari ambapo kampuni ya Microsoft haitakuwa na msaada ama wa bure au wa kulipia dhidi ya hali hiyo,kwani itakuwa imeshaacha kutoa msaada wa kuhusu Window XP
Chanzo:Gazeti la Mwananchi
Popular Posts
-
KAMA HAUKUJUA BASI JUA Na MBUKE TIMES Neno HACKER makusudio yake haswa sio kumaanisha mtu anayefanya vitendo vya kihalifu kwa kutu...
-
MTANZANIA ABUNI NA KUTENGENEZA PROGRAM TUMISHI YA KITABU CHA NYIMBO ZA KRISTO KATIKA VIFAA VYA APPLEMkurugenzi wa Mawasiliano wa Union Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania Gideo...
-
Kampuni ya vifaa vya kielektroniki, Samsung imeathiriwa na kushuka kwa mauzo ya simu zake za aina ya Smartphone. Mazingira mabaya ...
-
Zaidi ya wajumbe 26 kutoka Tanzania wamehudhuria kongamano la idara ya teknolojia ya habari na mawasiliano unaofanyika Nairobi nch...
-
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, Habari na Elimu kwa Umma wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisibwa akifafanua jambo wakati wa ki...
-
Akaunti ya Twitter ya kundi la wanamgambo wa Al Shabaab imesitishwa kwa mara nyingine. Ujumbe kutoka kwa Twitter katika akaunti yake ...
-
Kampuni ya Apple imezindua simu mpya aina ya iPhone X ambayo hutumia utambulisho wa uso wako badala ya kidole kufunguka. Apple imes...