Zaidi ya wajumbe 26 kutoka Tanzania wamehudhuria kongamano la idara ya teknolojia ya habari na mawasiliano unaofanyika Nairobi nchini Kenya chini ya viongozi wa mawasiliano wakanisa la waadventista wasabatao ulimwenguni.
Kongamano hilo lililoanza leo mjini Nairobi, linahusisha viongozi wa idara ya mawasiliano wa nchi kumi za afrika mashariki na kati malengo yakiwa ni kuelimishwa na kupewa mafunzo ya uinjilisti kupitia mtandao,kuzijua teknolojia mpya za kanisa la waadventista wasabato,namna ya kuzalisha video bora,jinsi ya kuwa na tovuti za aina moja za kiadventista,uhusiano wa umma,uhamaji kutoka analojia kwenda dijitali na matumizi ya michezo ya kompyuta kwa wokovu.
Mkutano huo unaohudhuriwa na wajumbe 76 kutoka nchi kumi za afrika mashariki na kati unaendeshwa na Mch Benjamini Schoun ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato ulimwenguni, Mkurugenzi wa Idara ya Program tumishi za Kanisa la Waadventista wasabato Ulimwenguni John Becket, Gideoni Mutero ambaye makamu mwenyekiti wa Hope Channel,Mhandisi wa mifumo ya Kompyuta wa Radio ya Waadventista Ulimwenguni Daryl Gungadoo na Sam Neves mtengenezaji wa program tumishi ya michezo ya kompyuta iitwayo heroes the Game.
Mkutano huo utahitimishwa machi kumi na tatu mwaka huu.