Tuesday, March 18, 2014

TCRA YASEMA WANANCHI WENGI HAWANA UELEWA WA HAKI ZAO KATIKA HUDUMA ZA MAWASILIANO

Imeelezwa kuwa wananachi wengi bado hawana uelewa wa kutosha juu ya haki zao za msingi katika huduma za mawasiliano wanazotumia, hali ambayo imekuwa ikisababisha wengi wao kuendelea kudhulumiwa haki zao bila kujijua.

Hayo yameelezwa hivi karibuni na Naibu Mkurugenzi Mratibu wa ofisi za Kanda Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA),Victor Nkya wakati akizungumza kwenye mkutano uliowashirikisha waalimu katika chuo cha ualimu Monduli katika kuadhimisha siku ya walaji duniani.


Bw Nkya amesema kuwa,bado uelewa ni mdogo sana kwa watumiaji juu ya haki zao katika matumizi ya mawasiliano , hivyo elimu zaidi iendelee kutolewa kwa watumiaji ili waweze kuzijua haki zao na kuweza kuzidai pale wanapokuwa wameonewa.


Naye Meneja wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kanda ya kaskazini , Annet Matindi amesema kuwa, watumiaji wa mawasiliano wanapaswa kuelewa haki zao za msingi na kuzidai haraka endapo wanahisi kuonewa kama vile kupata bili tofauti na matumizi yao ya mawasiliano wanayotumia na endapo hawataridhika wana haki pia ya kukata rufaa kuidai haki hiyo.


Matindi amesema kuwa,wamekuwa wakishirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo serikali na watoa huduma huku wakihakikisha kuwa mitambo ya mawasiliano

Popular Posts

Labels