Tuesday, March 18, 2014

CIA WANAFUATILIA TWEETS MILIONI 5 KWA SIKU



Shirika la kijasusi la Marekani,CIA,Kwa Mara nyingine limeripotiwa kufuatilia mitandao ya kijamii na kwamba kila siku mawakala wake wanasoma ujumbe milioni tano unaotumwa kwenye mtandao wa twitter tu.

Imekuwa ikiripotiwa kuwa Marekani ina utaratibu maalum wa kufuatilia Mawasiliano kutoka kwenye mitandao mbalimbali ya kwenye internet ,mbali na yale ya simu.

Shirika la Habari la AP,liliwahi kulipoti kuwa kati ya watumiaji  zaidi ya milioni 800 wa facebook na twitter ,taarifa milioni 400 zinazotumwa kwenye mitandano hiyo zinafanyiwa kazi na timu ya ufuatilia ya CIA.

Inaelezwa kuwa tweets hizo huwasaidia kufuatilia taarifa za kufahamu ‘mood’za watu katika jambo fulani na hivyo kutoa picha ya kinachoendelea kwa ikulu ya White House.
Lakini pia CIA wanatajwa kuitumia mitandao hiyo hiyo kwa ajili ya kupima upepo katika jambo fulani ,ili kubaini mwitikio wa watu wakoje.

Mfano unaotolewa katika hilo ni hatua yake ya kusambaza kwenye mitandao hiyo ya kijamii picha ya kuuawa kwa Osama bin Laden.

Mtandao wa kijamii wa twitter ambao ni miongoni mwa mitandao 10 maarufu duniani ulioanzishwa na Jack Dorsey ndio unaoonekana kutumiwa na watu wazima hasa maarufu duniani.

Tovuti ta statistic brain Twitter katika takwimu zake za januari mosi mwaka 2014 zinaonesha kuwa ulikuwa na watumiaji karibu milioni 646 na hadi kufikia mwaka 2013 ulikuwa umepata dola za kimarekani milioni 405 kutokana na matangazo ya biashara.

Popular Posts

Labels