Kabla ya kuanza kwa mkutano huo mapema asubuhi ya tar. 14 - 03 - 2014 |
Waandalizi wa mkutano wa maswala ya ulinzi mtandao wakiwa katika mapunziko ya chakula cha mchana kabbla ya kuendelea katika sehemu ya pili ya mkutano huo. |
Yusuph Kileo (katikati)akiwa pamoja na Bwana Craig rosewarne na Martin Euchner kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano |
Wadau wakifuatilia mkutano huo . |
Mkutano wa maswala ya ulinzi mtandao umemalizika kwa kuweka mkakati wenye kauli mbiu ya Mwaka 2014 ni wa vitendo
Akizungumzia
mkutano huo bwana Yusuph Kileo ambaye aliongoza timu ya maandalizi ya mkutano
huo alibainisha hayo na kueleza mkutano huo umekamilika salama ambapo mambo
mbalimbali yalipata kujadiliwa yahusuyo ulinzi mtandao “Cyber security” na
kupigilia msumari kauli mbiu ya mwaka 2014 kua ni mwaka wa vitendo.
Mwanzo
wa mkutano bwana Craig Rosewarne (Mwenyekiti wa kundi linalojiuhisisha na maswala
ya ulinzi mtandao (ISG) katika nchi za afrika ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa
kampuni Wolfpack inayo jihusisha na maswala ya ulinzi mtandao na mkurugenzi wa
SANS ukanda wa nchi za Afrika na mashariki ya kati) alianisha hali ilivyo sasa
na kusema kumekua na wimbi kubwa la makosa mtandao ambapo kila mwaka yanaongezeka
kasi huku akitolea mifano mbali mbali ya matukio ya hivi karibuni.
Aidha
alipata kuanisha ukuaji wa teknologia ambapo inaendelea kukua kwa kasi na inavyo
ongeza uwezekano wa kasi ya uhalifu mtandao kukua endapo jitihada za dhati
hazitowekwa tayari ili kukabiliana na changamoto zinazo rudisha nyuma vita
dhidi ya ulinzi mtandao.
Akitolea mifano changamoto mbali mbalizinazopelekea
ugumu katika ulinzi mtandao alianisha
changamoto hizo ikiwa ni pamoja na:-
1. Uhaba
wa programu za kompyuta salama kimtandao huku akitolea mifano baadhi ya program
za komputa zinavyo tengenezwa kutoa mwanya kwa wahalifu kupa urahisi kuingilia
komputa za watumiaji wa program hizo
2. Kutokuwepo na makubaliano ya pamoja ya
kisheria katika mapambano dhidi ya
makosa mtandao.
3. Kutokuwa
na ushirikiano wa kuunganisha nguvu kati ya serikali mbali mbali na sekta
binafsi kutokomeza uhalifu huu ambao unaendelea kukua kwa kasi.
4. Kutokua
na elimu kwa jamii juu ya makosa mtandao na jinsi ya kukabiliana nayo katika
ngazi ya ya mtu mmoja mmoja.
5. Kutokuwepo
na utayari kwa kuunda timu katka nchi mbali mbali zenye uwezo wa kukabiliana na
uhalifu mtandao.
Kwa
upande mwingine Bwana Martin Euchner kutoka ITU (International
telecommunication union) wakala wa umoja wa mataifa inayoshughulikia maswala ya
mawasiliano alianisha hatua mbali mbali mbali ambazo hadi sasa ITU imekua
ikizichukua ili kujaribu kuunganisha nchi zote za umoja wa mataifa ili
kwapamoja ziweze kupambana kupunguza uhalifu mtandao.
Pia
alipata kuzungumzia jitihada za dhati na mafanikio yaliyo patikana kupitia
mpango wa COP (Child Online Protection) ambao umejikita kuhakiki watoto
wanabaki salama mtandaoni, kauli iliyo ibua hoja nzito ya mchezo unao patikana
kwenye simu hivi sasa ujulikanao kama “Talking angela” ambao umekua unachezwa
na watoto wengi wadogo mtandaoni mchezo ambao umekuwa ukitiliwa shaka unaweza kuwa
unatumika vibaya na wahalifu mtandao ili kukusanya sauti za watoto na picha zao
zinazoweza kutumiwa vibaya baadae.
Aidha
bwana Eucner, aliweza kuzungumzia mpango kabambe ambapo mapitio na kuangalia
kwa karibu changamoto mtandao katika nchi mbali mbali katika mwaka huu wa 2014 zinategemewa
kufanyika katika nchi takriban 16 Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zitakazo
weza kufaidika na mpango huo.
Kwa
upande wa bwana Kileo, Aliweza kufafanua kwa kina uhaba mkubwa wa wataalam wa
maswala mtandao katika ngazi ya kidunia kwa sasa na mahitajio ya wataalam
imekua ni kubwa huku akitolea mfano katika nchi zilizo endelea kuwa na mikakati
kabambe ya kuunda jeshi Mtandao ili kukabiliana na vita mtandao maarufu kama
“Cyber war”.
Aidha Bwana Kileo aliasa washiriki kuendelea kufahamu yakua swala la mitandao ni
swala lisilo na mipaka ya kijografia na linaweza kufanywa na mhalifu kutokea
maeneo yoyote bila kujali anadhuru nchi gani hivyo nguvu ya pamoja ni muhimu
sana ili kuweza kukabiliana na hali mbaya iliyo sasa.
Katika
kusisitizia kauli hiyo ya bwana Kileo, Bwana Rosewarne alieleza ni swala lililo
wazi kuwa kwa sasa tatizo lipo hakuna ubishi huku akianisha hatua mbali mbali
zilizochukuliwa hadi sasa kukabiliana na uhalifu mtandao ikiwa ni pamoja na:-
1. kuwepo
na tovute maalum “ Alert website” ambayo itakua inatoa elimu kwa mwananchi
dhidi ya makosa mtandao.
2. Katuni
(Animation Video) ambazo tayari zimefikia 12 zinazotegemewa kuendelea kutumiwa
katika televisheni ili kutoa elimu kwa jamii dhidi ya maswala mtandao.
3. Upatikanaji
wa “phishing Task force” ambapo itajikita kukabiliana na makosha ya udanganyifu
mtandaoni maarufu kama “Phishing”
4. Kuendelea
kuangazia na kutengeneza “Action plan” kwa nchi za afrika na mataifa mengine
kiujumla kuziwezesha kukabiliana na makosa mtandao, huku akitolea mfano wa
kukamilika kwa zoezi hili katika mwaka huu kwa nchi ya Nigeria.