Friday, August 9, 2013

SONY NA PANASONIC WAUNGANA KUTEGENEZA CD YENYE UWEZO WA HIFADHI YA GB 300.



 
 Na Brown Nyanza
Kampuni mbili maarufu duniani SONY Corporation na PANASONIC Corporation kupitia tovuti zao wametangaza kuwa wameingia katika makubaliano ya kutengeneza CD (compact disk/Optical Disc) zenye uwezo wa kuhifadhi GB 300 za data ifikapo mwaka 2015.
Kampuni zote mbili zimeongeza kwa kusema kwamba hii itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya CD duniani. Katika miaka ya karibuni CD zimesifika kuwa na uwezo wa kuhifadhi data kwa ulizi wa hali ya juu, hii ni kutokana uwezo mkubwa wa kuhimili  mabadiliko mbalimbali ya kimazingira, vumbi, joto, na pia CD inaweza kuhifadhi  data kwa kipindi kirefu sana iwapo ikihifadhiwa sehemu nzuri.
Kampuni hizo zimekaririwa kwa kusema kwamba wateja wao hasa wamelengwa kuwa makampuni makubwa ya kutengeneza filamu nchini marekani na duniani kote, Pia makampuni makubwa ya utangazaji, Pia (Cloud based Data centes) zinatarajiwa kuwa ndio soko kubwa katika teknolojia hii mpya ya kuhifadhi data. Katika miaka ya karibuni Kampuni ya SONY ilitengeneza CD zenye zinazotumia teknolojia ya BluRay zenye uwezo wa kutunza data kwa kiasi cha GB 25 hadi GB 50 katika CD moja tu.

Popular Posts

Labels