Kampuni ya Huawei ya Tanzania imesaini makubaliano na Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST) kuhusu kukijengea chuo hicho uwezo zaidi wa kufanya tafiti katika masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA).
Katika makubaliano hayo,kampuni itakuwa ikitoa Dola 30,000 za Marekani kila mwaka ndani ya miaka mitatu,ili kusaidia chuo nyanja hiyo na hasa kwa wanachuo wa ngazi za uzamili na uzamifu.
Balozi wa China nchini Tanzania,Lu Youqing amesema moja ya mahitaji ya vyuo vinavyofanya tafiti duniani ni kupata vitendea kazi na wataalamu waliobobea.