Wednesday, November 25, 2015

VIKAO KAZI KWA WATENDAJI WA UMMA NCHINI TANZANIA SASA KUFANYIKA KWA KUTUMIA TEKNOHAMA



 

Serikali ya Tanzania  kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais imesema haitagharamia gharama zozote za kuendesha vikao kazi na watendaji wake kuanzia sasa, badala yake vikao hivyo vitaendeshwa kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKINOHAMA). 

Wahusika wakuu wa vikao kazi hivyo ni pamoja na Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Florence Temba, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, amesema kuwa, kupitia utaratibu huo washiriki wa vikao hivyo watabaki katika maeneo ya kazi ambapo wataunganishwa na mtandao wa pamoja kwa mfumo wa kuonana na kuongea uso kwa uso.

Aidha amewatoa hofu watumishi Kuhusu miondombinu ya mawasiliano kwa kusema Mfumo huo ni salama hakuna haja ya kuhofia kuhusu kukatika kwa umeme au hali ya hewa kwani mpango huo unaratibiwa na serikali hivyo ikitokea hali kama hiyo kutakuwepo na umeme wa ziada au kwa kutumia mkongo wa Taifa wa mawasiliano.

Monday, November 16, 2015

WANAFUNZI WA VYUO KUFURAHIA HUDUMA YA KUPIGIANA SIMU BURE TOKA TIGO

Meneja Mauzo wa mkoa wa Tanga kutoka Tigo Bw.Daniel Mainoya akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali , kuhusu uzinduzi wa kifurushi kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo katika Uwanja wa chuo cha Utumishi wa Umma, Kange, mjini Tanga.
Mwanafunzi kutoka chuo cha Utumishi wa Umma, Kange,mjini Tanga, Bi.Stella Mwakiliku akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali  kuhusu vipi wanafunzi wamekikubali kifurushi hicho kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo.

  1. Mwanafunzi kutoka chuo cha Utumishi wa Umma, Kange, Bw.Albert Risala akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu vipi wanafunzi wamekipokea kifurushi hicho kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo.
      Kikundi cha sarakasi  kikitumbuiza wanafunzi  katika uzinduzi wa kifurushi cha University pack kilichoboreshwa katika uwanja wa chuo cha Utumishi wa Umma,Kange, mjini Tanga.
Msanii wa kizazi kipya Roma Mkatoliki akiwatumbuiza wanafunzi wa chuo cha Utumishi wa Umma,Kange, mjini Tanga,katika uzinduzi wa kifurushi cha University pack kutoka Tigo kilichoboreshwa.


 Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imezindua kifurushi maalum kinacho wawezesha wanafunzi, ambao ni wateja wa Tigo, kuweza kupigiana simu bure.

Huduma hii imeboreshwa zaidi baada ya kifurushi hicho kwa jina maarufu kama Tigo Uni Pack kuzinduliwa mwaka jana, ukilinganisha na kifurushi cha zamani, kifurushi hichi kipya cha wiki kitawapatia wanafunzi wepesi wa kujiunga wakiwa popote ndani ya nchi, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kampuni ya Tigo leo.

Kinachohitajika ili wanafunzi waweze kutumia huduma hii,ni kuhakiki kwamba wamesajiliwa kama wateja wa Tigo katika Vyou vyao, ujumbe huo ulisema.

Akizungumzia kifurushi hicho kilichoboreshwa, Meneja wa Bidhaa kutoka Tigo Edwin Mgoa,alisema kifurushi hicho cha Uni Pack, kinadhirisha vipi Tigo inavyowasaidia wanafunzi kwa ajili ya kuwawezesha kuweza kupata huduma za mtandao za maisha ya kidijitali.

Baadhi ya huduma za kidijitali zinazotelewa na Tigo ni upatikanaji wa muziki bila kikomo kwa kupitia huduma ya Tigo Music, Facebook ya Kiswahili, Tigo Pesa App, Tigo Backup- huduma inayowawezesha wateja wa Tigo kuweza kurudisha simu na  zinapoibiwa au kupotea.

Kujisajili kwa kifurushi cha Uni Pack, mwanafunzi atahitajika kupiga *148*01*20#, namba ambazo kwa mujibu wa taarifa hiyo, imejumuisha vifurushi vingine muruwa kutoka Tigo.

VODACOM YAPELEKA SOMO LA ICT SHULE ZA SEKONDARI VIJIJINI


Baadhi ya Kompyuta zilizotolewa na Kampuni ya Vodacom kama msaada wa shule ya sekondari ya Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini.
Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini ,Henry Tzamburakisi akizungumza jambo na mkuu wa shule ya sekondari Shimbwe,Jacob Costantine alipotembelea darasa la Kompyuta shuleni hapo.
Mmoja wa wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la Learning Insync  akijaribu kuunganisha nyaya katika darasa la kompyuta lilopo shule ya sekondari Shimbwe iliyopo Uru wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakisi (kushoto) akiwa katika darasa la Kompyuta katika shule ya Shimbwe Sekondari ,wengine ni baadhi ya walimu katika shule hiyo ambao wamepatiwa mafunzo ya kompyuta.
Lisa Wolker akitoa maelekezo kwa walimu na wanafunzi.
Walimu na wanafunzi katika shule hiyo wakisikiliza kwa makini.
Mafunzo juu ya matumizi ya Programu maalumu ya kufundishia na kujifunzia yakiendelea katika darasa la Kompyuta katika shule ya sekondari ya Shimbwe.
Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Tzamburakisi akielekeza jambo kwa wanafunzi.
Jumla ya Kompyuta 30 zimetolewa na Vodacom kupitia mfuko wa Vodacom Foundation kwa shule ya sekondari Shimbwe ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa wataalamu wanao toa mafunzo ya matumizi ya Programu maalumu za kufundishia katika shule hiyo.

Wednesday, November 4, 2015

ALICHOANDIKA RAILA ODINGA MASAA SABA YALIYOPITA KWENYE TWITTER NA FACEBOOK KUHUSU RAIS MSTAAFU BENJAMINI MKAPA



SERIKALI YA TANZANIA YAKANUSHA TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA



Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa amefariki Dunia. 

Akizungunza na waandishi wa habari Hii leo katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwambene amesema Rais Mkapa yupo salama na mzima wa afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua.

Mwambene amewaasa watumiaji wa mitandao mbalimbali hasa Blogs kuacha kuitumia mitandao hiyo kwa kupotosha umma na kuandika mambo yasiyo na ukweli ili kuepusha mifumuko ya habari za upotishaji.

Aidha amesema Serikali italishughulikia hili na tayari imeshaanza kukamata baadhi ya watu mbalimbali ambao wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma kupotoka.

Amesema kuwa vyombo vya habari vifanye kazi kwa uweredi ili kazi ya uandishi wao iwe ya usawa na kufuata misingi ya uandishi, jambo ambalo wengi hukiuka kutokana kutofuata weredi wa kazi zao.

Popular Posts

Labels