Wakati
bado mafanikio mbali mbali yakijadiliwa wahalifu mtandao wamegundulika kuja na
uhalifu unaotafsiriwa kuwa ni wa kihistoria na uliofanyika kwa ubunifu na
umahiri wa hali ya juu ambapo wahalifu mtandao wamefanikiwa kusambaza kirusi
aina ya ModPOS kinacho athiri mashine zinazotumika kukamilisha miamala wakati
wa manunuzi.
Kirusi
cha ModPOS, kimegundulika Nchini Marekani wakati wa sherehe za “Thanks Giving”
ambapo watu wengi hufanya manunuzi. Kirusi hicho Kimekua kikifanikisha upotevu
mkubwa wa pesa wakati wa miamala.
Mara
baada ya ugunduzi huo wa ModPOS, mijadala kupitia mtandao ilianza baina ya
wanausalama mitandao ili kuweza kufanikisha mambo makubwa matatu. Moja ni
kuweza kugundua chanzo na jinsi ilivyo fanikishwa kuwepo bila kugundulika
(Inaaminika kimedumu muda – Taarifa ambazo bado zinafatiliwa) Pili, Ilikua ni
kutafuta suluhu ya kirusi hicho ili kiweze kuondolewa na Tatu, ni kupanga namna
ya kukuza uelewa wa namna ya kujikinga na janga hili la ModPOS.
Hadi
sasa bado hapajapatikana suluhu na inahofiwa huwenda kutokana na sherehe za mwisho
wa mwaka kirusi hicho kusambaa maeneo mengine huku mataifa yakitakiwa kuchukua
tahadhari. Inakadiriwa kama kitaendelea kutopatiwa suluhu; pesa nyingi
zitaishia mikononi mwa wahalifu mtandao na hasara itakayopatikana ni kubwa
zaidi kupata kutokea.
Wakati
hayo yakiendelea kuwa ni mjadala wa vuta nikuvute. Wahalifu wakadukua Kampuni
ya VTech inayotengeneza midoli ya watoto ya kielektroniki kutumia TEKINOHAMA ambapo
walifanikiwa kuiba taarifa zaidi ya milioni tano ikiwa ni pamoja na Picha za
watoto, Mawasilianao ya watoto na wazazi wao, Sauti za watoto, na taarifa za
miamala wakati wa manunuzi.
Inaaminika
kutokana na umakini mkubwa wanausalama mtandao wamekua wakiweka juu ya
kuwalinda watoto wawapo mtandaoni kitu ambacho kimepelekea kua na program ya
kidunia maarufu kama “Child Online Protection – COP” yenye dhamira ya kuhakiki
watoto wanabaki salama watumiapo TEKINOHAMA/ Mitandao, Wahalifu walitumia udukuzi
wa VTech ili kuhamisha mawazo ya kukabiliana na ModPOS na badala yake nguvu kubwa
ihamie kwenye udukuzi VTech.
Kufuatia
udukuzi huo kwenye kampuni ya VTech wanausalama mtandao walishauri Kampuni hiyo
kusitisha huduma zake za mtandao mara moja na kuendelea kutafuta suluhu ya
tatizo. Huku kampuni hiyo ikitakiwa kuhakiki taarifa zilizo dukuliwa hazipatikani/
kusambwazwa mitandaoni. Kampuni ya VTech tayari imechukua uamuzi wa kusitisha
huduma zake mtandao.
Hayo
yakijiri, Nchini Kenya nako wameshatoa Ripoti/taarifa za mwaka kuhusiana na
uhalifu mtandao ambapo uhalifu mtandao umeonekana kukua zaidi. Taarifa ilifafanua
uhaifu mtando umebadili taswira na kuwa si tu wa kudukua maneno ya siri bali ni
taarifa zinazoweza kupelekea mabilioni ya dola kuishia kwa wahalifu mtandao.
Jitihada za dhati zimeendelea nchini Kenya ili kukabiliana na uhalifu huu
mtandao.
Tanzania
nayo haijabaki salama, Baada ya uhalifu mtandao maarufu kwajina la “vikoba”
ulioshika kasi kipindi kifupi cha nyuma uliosababisha waathirika kuibiwa fedha
zao na wahalifu mtandao. Baadae elimu juu ya uhalifu huo ilisambaa na hatimae
kupungua sasa wahalifu mtandao wamekuja na aina mpya ya uhalifu mtandao wenye
dhamira ya kuiba taarifa za watu baada ya kufanikiwa kutengeneza program yenye
kuwashawishi watu kuingiza taarifa za wengine kwa madhumuni ya kudukua taarifa
za watu binafsi.Ikumbukwe hili ni kosa na lazima wananchi wawe makini kwenye hili.
Aidha, wahalifu
matandao wajakomea hapo, Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni ya kiusalama mtandao
ya “Symantec” imefanikiwa kugundua mbinu ambayo wahalifu mtandao wamekua
wakitumia mtandao wa kijamii wa “LinkedIn” ambapo wahalifu wamekua waki
dhamiria zaidi kuiba taarifa zinazopatikana kwenye mtandao huo baada ya kuweka
ukaribu na watumiaji mtandao huo kwa kuwaomba urafiki na baadae kutumia taarifa
zilizopo huko kufanya udukuzi.
Hili
tayari Symantec kwa kushirikiana na LinkedIn imeanza opareheni funga akounti
zozote zinazobainika kuwa ni za wahalifu mtandao na tunategemea kupata taarifa
yake kamili hapo baadae.
Matukio
hayo na mengine yanayowea kujitokeza watai tunaelekea mwisho wa mwaka ushauri
mkubwa umeendelea kutolewa ku kuhakiki panakua na mpango endelevu wa kukuza
uelewa wa matumizi salama ya mitandao (Cybersecurity awareness).
Pamoja na hilo mataifa yana aswa kua na tabia
ya kuhakiki yanatambua kwa ukaribu sana viashiria vyovyote vya kihalifu mtandao
ili kuweza kuweka mataifa yao salama kimtandao. Zaidi ni pamoja na kukuza nguvu
kazi watu kwenye sekta ya usalama mtandao pamoja na kua na matumizi ya watu sahihi katika
kukabiliana na uhalifu mtandao.
Natoa
wito wa kutambua uhalifu mtandao upo na una madhara makubwa katika sekta zote
kuanzia Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa, nakadhaika endapo hatua kuanzia ngazi ya
mtu binafsi hazitachukuliwa ili kuhakiki pana patikana usalama katika mitandao.
Tujenge tabia yay a kutafakari kabla ya kutumia mitandao ili kuhakiki hatusababishi
madhara kwa kuanzia kwa mtu binafsi pamoja na kwa wengine.
Na:Yusuph Kileo